Wednesday, May 18, 2016

IRAN YADAI KIM KARDASHIAN ANATUMIWA NA MAJASUSI KUPUMBAZA VIJANA NA WANAWAKE

* Watilia shaka umaarufu wake  Instagram

Taasisi iliyopewa jukumu la kulinda mfumo wa Uislam na kuzuia kuingiliwa na tamaduni za nje nchini Iran, The Iranian Revolutionary Guards Corp imemtuhumu Kim Kardashian West, 35, kuwa anafanya kazi katika mtandao wa kijamii wa Instagram ikiwa ni mkakati wa kupumbaza tamaduni, mfumo wa maisha na taifa la Kiislamu kwa kuwalenga vijana na wanawake kwa kuweka picha zinazokiuka maadili na taratibu za Uislam.

Kwa mujibu wa ripoti ya Iran Wire, tovuti ya habari inayoendeshwa na kundi la waandishi wa habari nchini Iran, kitengo cha taasisi ya kupambana na uhalifu mitandaoni imemlenga Kim Kardashian West ambaye ni mke wa msanii maarufu wa muziki wa Hip Hop Kanye West katika kipindi cha jumapili usiku.

“Bi. Kim Kardashian ni mwanamitindo maarufu, hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Instagram anamwambia ‘fanya mambo’” msemaji wa kitengo hicho, Mostafa Alizadeh alisema. “Hakuna shaka kuwa msaada wa kifedha unahusika pia. Tunalichukulia jambo hili kwa uzito mkubwa.”


Wakati anaongea na jarida la People, Cannes, Ufaransa, Kim alisema naye pia ndio kwanza anazisikia tuhuma hizo. “ndio kwanza nimetua( uwanja wa ndege) kuja hapa, sijasikia hiyo. Asante kwa kufuatilia.” Aliongea Kim Kardashian West.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Alizadeh alidai lengo la Mkurugenzi wa Instagram, Kevin Systrom ni kufanya Iran kuwa ni mahali pa mitindo ya mavazi na kuwa Kim anamsaidia kutekeleza azma hiyo.

“wanawalenda vijana wadogo na wanawake,” alisema Alizadeh kwa mujibu wa Iran Wire. “Wageni pia wanahusika sababu wanalenga familia. Kitovu cha mfumo huo ni kutoka Gulf ya Persia na Uingereza. Ukichora mpango mkakati huo, utaona kuwa ni mkakati kutoka nje.”

Matukio hayo ni mkakati maalu wa kupiga vita uhuni na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook, kuvunja ushabiki wa kisiri na uendeshaji wa Instagram “yenye lengo la kuzamisha utamaduni wa maisha ya Uislam nchini Iran” ilieleza Iran Wire.

Baadhi ya wanawake nchini Iran wameripotiwa kukamatwa, Iran Wire ilimkariri Javad Babaee, kutoka katika ofisi ya Mwendesha Mashitaka, kuwa waliwaonya watu zaidi ya 170, huku 29 wakilengwa kuhukumiwa.

“lengo letu ni kuwafundisha na kuwaamsha” Babaee anadaiwa kusema.

Hata hivyo baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Instagram waliotajwa kulengwa bado wanendelea kupatikana katika mtando huo katika kurasa za Elnaz Glrokh na Hamid Fadaei, japokuwa wamiliki wake wameshaondoka Iran.




No comments:

Post a Comment