Sunday, April 24, 2016

PAPA WEMBA AMEFARIKI, ANGALIA VIDEO ALIVYOANGUKA JUKWAANI





Mwanamuziki maarufu barani Afrika na gwiji la muziki wa rumba ameanguka akiwa jukwaani anaimba na kisha kupoteza maisha.

Kwa mujibu wa Mirror Online, Mwanamuziki huyo kutoka Kongo, Papa Wemba alikuwa anaimba katika tamasha jijini Abidjan nchini Ivory Coast ghafla alianguka. Video inaonesha waimbaji na wanamuziki wenzie wakimkimbilia kumsaidia, baadae vyombo vya habari nchini humo viliripoti kuwa Papa Wemba amefariki akiwa na miaka 66.

Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, ni mmoja wa wanamuziki mashuri na wanaojulikana sana barani Afrika. Alikuwa anaimba katika tamasha la muziki lijulikanalo kama Festival des musiques urbaines d’Anoumabo (FEMUA) alipozimia.


Waandaaji wa tamasha hilo baadae walitangaza walipokutana na waandishi wa habari. Msemaji wa tamasha hilo Henry Christmas Mbuta Vokia, alikiambia kituo cha Radio Okapi ya jijini Abidjan "Majira ya saa 11:10, kwa saa za Abidjan, Papa Wemba alitangazwa jukwaani. Aliimba nyimbo ya kwanza nay a pili, kisha akadondoka na kuzimia.”

“nilikuwa naangalia kwenye televisheni, nikaona waimbaji wenzie wamemzunguka Papa Wemba. Nikafikiri ni mbwembwe za jukwaani, lakini baadaye nikaona wafanyakazi wa Red Cross wakiingia jukwaani, ghafla tv ikakata matangazo, nikajaribu kumpiga simu Meneja wa Papa Wemba, Cornelie.

Akaniambia Papa Wemba kaanguka wakati anaimba jukwaani, nakumbuka dakika kumi baadae nikaambiwa yuko chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Nilipopiga nusu saa baadaye Corneli akaniambia Papa Wemba amefariki.”


No comments:

Post a Comment