Monday, April 25, 2016

ABLAMU MPYA YA BEYONCE 'LEMONADE' YAHUSISHWA NA KUCHEPUKA

Beyonce ametoa albamu mpya ijulikanao kama Lemonade na kuamsha hisia za mashabiki wake zenye madai yanayohusishwa na udanganyifu katika ndoa.


Na Mwandishi Wetu

Mitandao bado kidogo izidiwe nguvu na watumiaji jumamosi usiku baada ya msanii maarufu wa muziki wa nchini Marekani, Beyonce kuachia albamu yake mpya “Lemonade”. Kama ilivyokuwa albamu yake ya mwisho hii nayo imeleta hisia na maneno mengi.

Kwa mujibu wa CNN, kelele zinazopigwa sasa hivi hazina uhusiano na musiki, mtindo wake wa uvaaji au ubunifu uliotumika katika albamu hiyo. Badala yake ni mistari yake ilivyo na hisia za kutendwa na mpenzi wake kiasi cha kuamsha hisia kwa mashabiki wake.

Ukisikiliza albamu hiyo mwanzo mwisho, utasikia maneno yake ya kumlalamikia mume mwenye tabia ya kuchepuka, maumivu ya kuibiwa mume na malumbano ya wapenzi.


Mfano wimbo “Sorry” Beyonce anaimba "I see them boppers in the corner / They sneaking out the back door / He only want me when I'm not there / He better call Becky with the good hair." Akimaanisha “nawaona ‘wezi’ kwenye kona/ wakitokea mlango wa nyuma/ ananihitaji nikiwa sipo/bora amuite Becky mwenye nywele nzuri.”

Mwimbaji huyo ni mke wa msanii rapa maarufu Jay Z. mwisho wa video ya nyimbo hiyo inamuonesha Beyonce akiwa na Jay Z pamoja na mtoto wao Blue Ivy kwa pamoja wakiwa na furaha.

Sio kila wimbo unalenga matatizo ya mahusiano kwenye ndoa. ‘Lemonade’ inagusa hisia, mapenzi pamoja na umuhimu wa maisha ya mtu mweusi, na mwishowe Beyonce anatoa hadithi ya mwanamke asiyetaka mzaha.

Albamu hiyo ni nguzo ya mwanamke mweusi, pamoja na hadithi nyingi zinazomhusu mwenyewe. Beyonce ameweka video za baba yake, ndoa yake na Jay Z, ujauzito wake pamoja na siku ya kuzaliwa ya mwanae Blue Ivy.


No comments:

Post a Comment