Friday, February 05, 2016

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU UDAHALILISHAJI WA MWANAFUNZI WA KITANZANIA INDIA

(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)

Seriklaiimetoa tamko la kulaani kitendo kilichotokea nchini India kwa mwanafunzi wa kike wa kitanzania kuvuliwa nguo na kutembezwa barabarani ambapo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na kimataifa imetoa tamko la kulaani suala hilo kwa kuitaka Serikali ya india kuchukua hatua.

Akitoa tamko hilo Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Dkt Augustine Mahiga amesema ni kweli kwamba kuna mwanafunzi wa kike wa kitanzania alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji nchini India kwa kuvuliwa nguo na kutembezwa barabarani suala ambalo lilizua mijadala mikubwa nchini kuhusu udhalilishaji huo.

“Wizara yetu imezungumza na Balozi wa India nchini na kumweleza ni kwa jinsi gani watanzania wamefadhaika na kusononeshwa na kitendo alichofanyiwa mtanzania mwenzao huko India na Balozi alituhakikishia kwamba amewasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi yake na kusema Serikali ya India kwa kushirikiana na Jeshi la polisi nchini humo wamefanikisha kuwakamata wote waliohusika na kitendo hicho na kuwafikisha mahakamani kujibu mashataka hayo”

“ Pia Serikali ya India imeahidi kutoa ulinzi kwa wanafunzi wa kitanzania na wenye asilia ya Afrika wanaosoma huko ili kuwalinda na kuwaepusha na vitendo hivyo vinavyofanya na raia ambao hawana nia njema kwa mahusiano mazuri ya kimataifa yaliyopo kati ya India na Tanzania”Alisema Mhe. Mahiga.

Serikali ya Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na Serikali ya India kwa miaka mingi sasa na kutokana na kitendo hiki kilichotokea nchini India,Waziri wa Mambo ya Nje ya India amefatana na Balozi wa Tanzania nchini humo kwenda Mji wa Bangalo ili kuongea na wanafunzi wakitanzania na wale wenye asili ya Afrika wanaosoma huko ili kujenga mahusiano mazuri na wazawa ikiwa ni jitihada za kupunguza vitendo hivyo kutokea mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment