Katika post hiyo Lulu aliandika “The Ones Who Can't have you will always drag you to make themselves feel better..” akimaanisha “Wasioweza kukupata watakuburuza ili wajisikie vizuri”.
Msanii huyo maarufu wa filamu anayedaiwa kuwa ni mmoja kati ya wasanii wachache katika bongo movie anayelipwa hela ya juu zaidi katika project, aliandamwa hivi karibuni na maneno kwenye mitandao ya kijamii kufuatia ukaribu wake na msanii Techno kutoka Nigeria.
Lulu ni kati ya wasanii wachache nchini wenye uvumilivu mkubwa haswa pale anapoandamwa na maneno makali na uchokozi mwingi kutoka kwa mashabiki na wasiompenda.
“Lulu ni kati ya wasanii wachache sana wenye uwezo mkubwa wa kuvumilia, alishatukanwa mara nyingi sana kwenye mitandao ya kijamii lakini yeye hukaa kimya kama vile haya muhusu” alisema mmoja wa mashibiki wake alipohojiwa na Imma Matukio nakudai kutotaka kutajwa.
Shabiki huyo aliongeza kuwa akitukanwa na kusimangwa na maeneno yeye hupuuzia na kesho yake utaona kaweka bonge la picha yake akiwa na sura ya furaha katika maisha yake.
No comments:
Post a Comment