Tukio la kusikitisha lilimtokea msichana mwenye miaka 21,
Mtanzania saa moja na nusu jioni, Jumapili wakati akiwa na Watanzania wenzake
watatu walipokuwa kwenye gari Ganapathinagar, nje kidogo ya barabara kubwa ya
Hesaraghatta, Bengaluru, nchini India.
Ikiwa ni umbali wa kilometa 2 toka barabara kuu, nusa saa tu
baada ya gari alilokuwa anaendesha mwanafunzi Msudani alipomgonga mwanamke aliyejulikana
kama Shabana Taj, 35 na kupoteza maisha alipokuwa akitembea na mumewe Sanaullah
ambaye ni fundi umeme.
Kundi la Wahindi waliochukizwa na tukio hilo walisimamisha
gari alilokuwemo Watanzania hao. Akieleza katika mahojiano kwa uchungu, bindi
huyo alisema, “Tulitoka nje ya gari ambapo palikuwa na watu wengi wamezunguka
gari. Pembeni alikuwepo polisi amesimama, nilimuuliza kimetokea nini, akajibu
hakuna chochote. Rafiki yangu akanikimbilia na kuniambia nisisogee, wakati huo
kundi hilo lilianza kumpiga” alieleza msichana huyo.
“Wakanisukuma na
kuanza kunipiga, nilikuwa nimevaa t-shet. Wakaivuta na kuichanachana, na
kuniacha nikiwa mtupu. Wakaendelea kutudhalilisha tulipopata upenyo tukaanza kukimbia
ili kuokoa maisha yetu.” Alihadithia Binti huyo.
“Nikiwa na wenzangu tuliingi kwenye basi, dereva hakuendesha
badala yake abiria waliokuwemo wakatusukuma nje. Tukabakia mikononi mwa kundi
hilo.” “ndipo msamaria mwema akanipa tshirt, ambapo na yeye akashambuliwa,
waliendelea kutupiga mpaka tukaingia katika duka moja lililokuwa karibu”
alisema
Wakati huo baadhi yao walishawasha moto gari letu na kuanza
kulichoma na kuliteketeza. Wakati wanaelekea katika hospitali ya Sapthagiri, kundi hilo
liliendelea kuwafukuza, hata walipofika hospitali kundi hilo lilidaiwa kutishia
kuvamia hospitali hiyo kama Waafrika hawatatolewa nje.
Polisi imedai kuchukua maelezo ya msichana huyo jumatano,
wakidhibitisha kupata maelezo hayo na kuchelewa kulichukulia hatua tukio hilo
kwa siku tatu. Kiongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa kutoka Afrika, Bosco
Kweesi amelaumu ajali ililosababishwa na Msudani hiyo na kusababisha kifo cha Shabana
na kudai kuwa sheria ifuate mkondo.
Hata hivyo kushambulia watu kutokana na rangi yao ni jambo
la kupinga kabisa, aliongeza kuwa suala hilo linafanyiwa kazi pia na balozi za
nchi zote za Afrika wanazotoka wanafunzi hao.
Kweesi alisema, “ Mwanamke huyo amefariki na waliohusika na
ajali hiyo wachukuliwe hatua. Lakini hawa waliodhalilishwa hawahusiki kabisa na
tukio hilo”. Naye kiongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Tanzania alisema,
walikimbilia kituo cha polisi jumapili usiku, kutaka msaada ili wawapeleke
wenzao hospitali.
Alisema “ Polisi waligoma kutusaidia na hata kusikiliza
malalmiko yetu, wakati huo polisi walikuwa wanamshikilia mwenzetu ambaye
hausiani kabisa na tukio hilo. Polisi mmoja akatuambia kuwa nyie wote mnafanana
na mwezenu ataachiwa mkimleta dereva aliyesabababisha” alieleza.
“Sasa hivi tunamuogopa kila Muhindi anayetusogelea, baada ya
yaliyonikuta”, aliongea msichana huyo Mtanzania mwenye umri wa miaka 21
anayesoma City College wakati akiongea na waandishi wa habari katika hospitali
ya Sapthagiri, ambapo alipelekwa kwaajili ya vipimo mbalimbali.
Waziri wa Uhusiano wa Mambo(External Affairs Minister) ya
Nje Sushma Swaraj, akionesha kuwa na taarifa aliweka katika mtandao wa twitter
akisema “Tumeumizwa sana juu ya tukio la aibu alilofanyiwa msichana wa
Kitanzania huko Bengaluru”
Waziri huyo ameitaka serikali kuhakikisha usalama na ulinzi
kwa wanafunzi wote ambao ni wageni nchini humo. Katika taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania nchini
India ilimtaka Waziri Sushma Swaraj kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya
wale waliomdhalilisha msichana huyo.
Jumatano iliyopita Polisi wa Bengaluru walifungua kesi chini
ya kifungu 354 IPC dhidi ya watu ambao hawakufahamika, wakati ambapo watu wanne
walikamatwa jioni siku hiyo.
No comments:
Post a Comment