Monday, February 15, 2016

BEN POL NA JUX WAPEANA MAKAVU KWENYE 'NAKUCHANA'

PRESS RELEASE 



​Dar es Salaam, Tanzania

Ujumbe wenye dalili za ukweli uliojificha ndani ya mzaha umezaa wimbo mkubwa kati ya wakali wawili wa RnB Tanzania, Benard “Ben Pol” Paul ​na Juma “Jux” Khaleed.

​‘NAKUCHANA’ ni wimbo mpya wa RnB ambao ndani yake Ben Pol na Jux wanasikika wakipeana ‘makavu’ kuhusu mambo kadhaa hasi kuhusu wao, huku kila mmoja akitafuta kile anachoamini ni kona dhaifu ya mwenzake.

“Nakuchana ilizaliwa baada ya mimi na Jux kwenda studio, na tulienda studio tulitaka kwenda kurekodi kabisa wimbo rasmi, lakini tukawa tunajivuta vuta, tukaona bana eh hebu lets just have fun umeona, sababu tulikaa muda mrefu kama masaa matatu hatujapata kitu. Kwahiyo tukasema ngoja tujifurahishe (kwa kuchanana) kama watu ambao wanakuwa wana have fun wanavyochill sehemu, unajua wanazinguana wanafanyaje. Kwahiyo kwenye ku-have fun ndio tukaandika mstari mmoja mmoja tunau record, tunaandika mmoja tunau record yaani tumeandika yote kwa pamoja. Kwahiyo hivyo ndivyo ambavyo ‘Nakuchana’ ilivyozaliwa.” Alieleza Ben Pol kuhusu wimbo huo.
Ben Pol ameongeza kuwa wamelazimika kuitoa ‘NAKUCHANA’ kipindi hiki kutokana na demo ya wimbo huo kuvuja siku chache baada ya kurekodiwa na kuonekana kupendwa na mashabiki wengi.

‘NAKUCHANA’ ni wimbo uliopikwa ​na producer Bob Manecky wa studio ya A.M Records, na ndio collabo ya kwanza kwa Jux na Ben Pol kufanya.




No comments:

Post a Comment