Monday, February 01, 2016

AIRTEL FURSA KUTUMIA SIMU KUWAFIKIA VIJANA NCHI NZIMA



AWAMU ya pili ya mpango wa Airtel FURSA imezidi kujimarisha nchini baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kujipanga kutoa mafunzo ya ujasiriamali na kutumia mtandao wa Airtel kuwafikia vijana nchi nzima kwa njia ya simu.

Akizungumza jijini hapa mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano(Pichani Juu), alisema mafunzo yajayo ya semina zinazoendelea kwa vijana wajasiriamali yatafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Lindi.
“Pia wakati wowote kuanzia sasa Airtel FURSA tutaweka wazi mfumo wa mafunzo kwa njia mpya ya kiubunifu zaidi kwa njia ya simu za mkononi ili kuwafikia vijana wengi zaidi wanaokabiliwa na changamoto za ajira,” alisema Bi, Singano.

Alisema walengwa wa mpango huo ni vijana wenye kati ya umri wa miaka 18 na 24 na kwamba tangu mradi huo uanze mwaka jana na kudumu kwa miezi sita, takribani vijana 2,500 nchini wamekwishafaidika na sasa wanamiliki biashara na miradi mbalimbali.

Mkurugenzi huyo wa Airte Bi, Beatrice Singano aliwaomba wadau na serikali kujitokeza na kushirikiana na Airtel kuwawezesha vijana ili nao waweze kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka.

“Katika msimu huu wa pili wa Airtel FURSA, tutawafikia vijana wengi zaidi na kuwapa mafunzo na semina, ushawishi na kuwainua kwa misaada ya vitendea kazi.

“Tayari tumefika na kutoa mafunzo katika mikoa ya Manyara na Morogoro, sasa tunaingia Dodoma, kisha vijana wa Lindi na Dar es Saalam wajiandae,” alisema.

Alisema uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa njia ya simu utawezesha hata wale wasio na nafasi ya kuhudhuria mafunzo na semina, wataweza kufanya hivyo popote walipo.

“Tunaamini kuwa msimu huu utakuwa na mafanikio zaidi kwani wengi watawezeshwa kupitia programu hii,” alisema

Mpango wa Airtel FURSA ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa kuwapatia vifaa, mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kwa njia tofauti waweze kufikia malengo yao.

Pia mpango huu unawawezesha vijana kuongeza mitaji au kupanua biashara zao za ujasiriamali kwa kuwapa msaada wenye thamani ya hadi Sh. milioni 10 kwa kila mmoja.

Ili kijana kufaidika na msaada huo, anatakiwa kutuma maombi kwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenda namba 15626 akiwa jina kamili, umri wake, aina ya biashara anayoifanya, mahali alipo na namba za simu, au kupitia airtelfursa@tz.airtel.comau kujaza fomukutoka kwenye tovuti www.airtel.com.

No comments:

Post a Comment