Katika uchaguzi Mkuu uliofanyika leo saa tisa alasiri katika Hoteli ya Nashera mjini Morogoro ili kupata viongozi wa ngazi ya juu kabisa katika Jukwaa la Wahariri nchini, umekamilika huku Bw. Theophil Makunga akiibuka mshindi na kuwa Mwenyekiti mpya. Makunga anachukua nafasi ya aliyekuwa Bw. Absalom Kibanda, ambaye muda wake umekwisha pamoja na uongozi mzima wa Jukwaa.
Makunga ameshinda mpinzani wake Bw. Jesse Kwayu huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikienda kwa Deodatus Balile baada ya kumbwaga Bakari Machumu.
Safu mpya ya uongozi wa Jukwaa la Wahariri, kuanzia kushoto
walioketi ni Neville Meena( Katibu Mkuu), Theophil Makunga(Mwenyekiti),
Deodatus Balile(Makamu Mwenyekiti), Nengida Johanes(Katibu Msaidizi), safu ya
nyuma kutoka kushoto ni Wajumbe, Joyce Shebe, SAlim Said Salim, Bakari Machumu,
Jesse Kwayu na Lilian Timbuka
PICHA ZOTE NA IMMA MATUKIO
No comments:
Post a Comment