Historia inaonyesha panya walianza kufugwa nyumbanitangu karne ya 19. Wengi wakiwa ni panya wa kahawia lakini hata weusi na ‘Giant pouched rats’(wanaopatikana Jangwa laSahara) nao pia hufugwa.Panya wafugwao huwa na tabia tofauti ukilinganisha napanya wa mwituni kulingana na vizazi vingapi vimewekwa kama mifugo.
Hawa panya wafugwao,huwa hawaleti hatari sana ya magonjwa kama mifugo mingine, yaani paka na mbwa huwa marafiki na wanaweza kuzoeshwa kufanya kazi mbalimbali.
Panya wafugwao huwa watiifu na wasikivu kuliko panya wa kale, pia hupata magonjwa mara kwa mara kotokana na kuzaliana na jamii tofauti.
Panya wa kufugwa ni tofauti sana na wale wa mwituni. Ni wapole na hung’ata kwa nadra sana pia huvumilia uwepo wa watu wengi na huzaliana mapema na kwa wingi sana na ubongo, maini, mafigo, tezi ya adrenali na mioyo yao ni midogo sana. (Barnert 2002).
Tofauti na Panya wanaoishi mwituni ambao inaaminika kuwa wanaweza kubeba baadhi ya magonjwa na kuyapeleka kwenye mamalia wengine kwa mfano huko Ulaya katika miji kadhaa ugonjwa wa ‘Black Death’maarufu kama tauni uliua zaidi ya watu milioni 25 katika miaka ya 1348-1350 huku ikisemekana kuwa ulisabbishwa na vimelea vya yersinia pestis vilivyobebwa na kunguni wa panya wa tropiki waliokuwa
wanajishibisha kwa panya wengi wa huko Ulaya.
Hiyo imeendelea kwenye nchi nyingi kwani licha ya magonjwa ya binadamu pia panya wanahusishwa na
magonjwa ya mifugo kama vile homa ya ini ya nguruwe.Kwa kawaida panya huishi kwa muda wa miaka mitatu, lakini wengi huishi kwa mwaka mmoja tu kutokana na kuwindwa na wanyama wengine kama nyoka.
Kwa kawaida panya kama anavyochukuliwa na watu wengi kuwa myama mchafu, hatari na anayeweza kusababisha magonjwa bila kutambua kuwa kuna faida nyingi zinatokana na panya ambapo hutumika kama, KIUNGO CHA TAFITI:
Aina moja ya panya wa maabara inayojulikana kama panya Zucker,wao wanazalishwa wakiwa na uwezo wa kupata kifua kikuu na magonjwa mengine ya binadamu.Mfano 1895, chuo kikuu cha Clark, Worcester, Massachusetts(Marekani) kilianzisha kundi kubwa la panya weupe kwa ajili ya kujifunza madhara ya chakula na mapungufu mengine ya mwili.
Kwa miaka mingi panya wametumika kama viungo vya tafiti za magonjwa mbalimbali na kuongeza ufahamu wetu kuhusu viasilia, magonjwa na madhara ya madawa, na mada nyingine ambazo zimechangia kwa kiwango kikubwa kwenye masuala ya afya ya mwili wa binadamu.
Na hapa Nchini kwetu wamekuwa wakifundishwa kuchunguza magonjwa ya kifua kikuu na kuchunguza dalili za mapema katika mate ya binadamu Kutokana na uwezo wao wa kunusa harufu mara nane kwa
sekunde ikilinganishwa na mara mbili kwa binadamu. Panya pia ana uwezo wa kutambua harufu mbili kwa kunusa mara moja kwa mujibu wa chuo kikuu cha Sokoine Tanzania.
Na uchunguzi wa mwaka 2007 umebaini kuwa panya wana uwezo na akili ambapo hapo awali ulionekana upo kwa binadamu pekee na baadhi ya wanyama wa kale babu wa binadamu.
PANYA KAMA CHAKULA:
Imebainika kuwa nyama ya panya huwa ni chanzo kizuri cha protini kuliko nyama nyingine.Mfano huko Amerika ya Kusini baadhi ya watumwa wa kiafrika walitumia nyama hiyo kutosheleza milo yao,Australia
watu jamii ya Aborigines, wanatumia panya kwenye milo yao na huko India wanawake wa jamii ya Mishmi, hutumia panya sababu huruhusiwa kula nyama ya samaki, nguruwe na panya tu.
Aidha Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa lilikadiria kuwa zaidi ya nusu ya nyama inachotumiwa naWaghana ni panya na kwa Nchi za Magharibi huruhusu ulaji wa nyama hiyo tofauti watu wa jamii ya Shipibo (Peru) na watu wa Sirionó(Bolivia)wao ni marufuku kula panya.
Mathalani wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu nchini wameshauri kufuga na kula panya aina ya ndezi huku wakieleza kuwa nyama hiyo haina mafuta mengi, ikiwa pia na virutubisho muhimu na vilivyo adimu.
Pia panya hutumiwa kama chakula na nyoka, na wanyamawengine walao nyama. Ambapo jamii mbili za chatu hulapanya pekee na wengine huwafuga ili kulisha mifugo yao.
PANYA KAMA TAMADUNI:
Vilevile baadhi ya jamii katika nchi mbalimbali huwatumia panya kama kielelezo au sehemu ya utamaduni wao,kwa mfano Panya wa asili huruhusiwa kutembea huru kwenye Hekalu la Karni Mata(India)wanawawekwa kama wanaume watakatifu. Wahudumu huwalisha panya hao kwa nafaka na
maziwa na mtu akila chakula kilichoguswa na panya hao huonekana kama baraka toka kwa Mungu. .
Katika Nchi ya China, panya ni mmoja kati ya wanyama wa walio kwenye kalenda ya Zodiac ya wachina.Na wanaamini kuwa watu waliozaliwa kwenye mwaka wa panya huwa wana tabia za panya zikiwemo: ukweli, ukarimu, kiu ya kufanya mambo, hasira ya haraka na ufujaji.
Faida nyingine ya panya kutokana na utafiti uliofanywa na raia wa Ubelgiji,Bart Weetgen mwaka 1998 ambayo pia ni adimu kupatikana kwa wanyama wengine ukiacha mbwa ni kuwa panya ana uwezo mkubwa wa kunusa na kutegua mabomu yaliyotegwa ardini kwa umbali mrefu wa kipimo cha mita.Hiyo inatokana na udogo wa umbile lake pamoja na uzito humfanya asiweze kulipua mabomu ardhini pale anapoyabaini
na ili aweze kufanya kazi hiyo ni lazima apate mafunzo ambayo humpitisha katika hatua 9 mojawapo ikiwa kumfanya rafiki na kumjengea mazingira ya kumzoea mwanadamu.
Kiongozi Mkuu wa Mafunzo ya panya Nchini(SUA),Abdullah Mchovu,anaeleza sifa na tabia ya kipekee ya panya ni uwezo wa kuhifadhi na kufukua ."Kwa uasilia panya hukusanya mazao wakati wa mavuno,kisha kuyaficha katika mashimo shambani na baadaye wakati wa ukame hutumia njia ya kunusa ili kuyapata mazao waliyoyaficha,"Anaongeza kuwa "Sifa za kunusa ndizo zilizofanya wahakiki kumteua panya kuwa mteguaji bingwa wa mabomu kuliko binadamu au vifaa vya kiteknolojia.Ni nafuu zaidi kumtunza panya kuliko mbwa kwani wao wanafuata zaidi vitendo kuliko kufuata kinachofanywa na muongozaji,".
Hata hivyo itambulike kuwa pamoja na faida zote hizo lakini panya anatajwa kuwa ni chanzo kikubwa cha ongezeko la umasikini katika Nchi zinazoendelea hususani Tanzania.
Ni ukweli usiopingika kuwa kilimo ndio uti wa mgongo kwa nyingi za kiafrika na panya ni tatizo kubwa kwenye kilimo katika Bara la Afrika.Ambapo milipuko husababisha uharibifu mkubwa wa mazao
ya nafaka, Kituo cha kutafiti udhibiti wa viumbe hai waharibifu (SUA) kimeeleza kuwa uharibifu huo wa nafaka unakaribia asilimia 48, ambayo ni haraka kubwa kwa wakulima masikini.
Tanzania pekee hupoteza zaidi ya tani 400,000za mahindi kila mwaka,chakula hicho kinngeweza kutosha kulisha zaidi ya watanzania milioni 2 kwa mwaka mzima. Milipuko ya panya kulingana na utafiti wa kituo hicho ,huweza kusababisha hasara inayofikia asilimia 100 na husababisha matukio ya njaa kuongezeka kwa kiwango kikubwa katika jamii.
Kutokana na hali hiyo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Kituo hicho, kilianzisha mradi wa utafiti wa kudhibiti milipuko ya panya kwa kutumia vizuia uzazi.
Hatua ambayo pengine ni hatari kubwa kwa maisha ya binadamu na wanyama wengine kutokana na udhibiti wa panya hao kutegemea matumizi ya sumu ukiachilia mbali ya kuwa za gharama na hazimfikii mkulima wakati anapohitaji. Lakini pia utafiti uliofanywa na Shirika la Utafiti wa Sayansi na Viwanda la Australia (CSIRO), duniani kote panya kumi huzaliwa sawa na mtoto mmoja wa binadamu anayezaliwa.
Kila siku watoto 360,000 waliozaliwa karibuni wanahitaji kulishwa, wakati huohuo panya 3,600,000 waliozaliwa karibuni pia wanataka chakula.Kwa mfano, nchi ya Indonesia ina wakazi milioni 230 na asilimia 60 kati yao hula wali kila siku.
Hata hivyo, katika nchi hiyo panya hula asilimia 15 ya mazao ya mpunga kila mwaka. Mwanasayansi Dkt. GrantSingleton, mfanyakazi wa shirika la CSIRO anasema kuwa:“Jambo hilo linamaanisha kwamba panya hula kiasi cha mchele ambacho kingeweza kuwalisha Waindonesia zaidi ya milioni 20 kwa mwaka mmoja.”
Zipo njia mbalimbali zinazoweza kutumika ili kupambana na wanyama hao waharibifu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kitengo cha kuthibiti wanyama waharibifu,Profesa Loth Mulungu,njia kubwa na ya haraka ambayo pia haina gharama ni mkojo wa paka(jike) ambao umebainika kuwa na harufu kali inayowafanya panya wakimbie mara tu wanapoinusa kwa kudhani panya yupo eneo hilo tofauti na kutumia sumu.
No comments:
Post a Comment