Friday, November 27, 2015

MAHAKAMA TANZANIA BEGA KWA BEGA NA WAANDISHI WA HABARI

Jaji kiongozi wa Mahakama kuu ya Tanzania Shaaban Lila amesema kuwa majaji wa Tanzania wanabusara katika kufanya maamuzi yao na ndio maana hata vyombo vya habari nchini hata vinapowachafua hawaangaiki kufikisha kwenye vyombo vya dola.

 Jaji kiongozi huyo amesema hayo leo wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili  kwa waandishi wanao ripoti habari za mahakamani yaliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo zaidi wa kuripoti habari za mahakama.

"Si uoga bali ni busara zinazotumika kwa majaji kutosumbuana na vyombo vya habari pale waandishi wanapotoa taarifa za maamuzi ya hukumu katika kesi zenye mvuto wa jamii ambazo zinaashiria kama majaji wanapendelea upande mmoja."alisema

Aliongeza kuwa majaji wana mioyo ambayo inasikia uchungu kama binadamu wengine pale wanapoandikwa ndivyo sivo wakati wanapokuwa wakisikiliza na kutoa maamuzi ya kesi mbalimbali.
Alisema kuwa majaji kama wasingekuwa na busara wangefungua kesi nyingi mahakamani dhidi ya vyombo vya habari kutokana na vichwa vya habri vya magazeti kwa namna vinavyoandikwa ndivyo sivyo.

"Tungefungua kesi nyingi dhidi ya vyombo vya habari kwa kutuandika habari ambazo si sahihi huku wakishambulia majaji jambo ambalo halileti picha nzuri kwa jamii na kupelekea jamii kutoaiamini mahakama."alisema

Alisema kuwa mahakama haikwepi kuambiwa kasoro za kiutendaji wa kazi zake na kwamba wapo tayari kupokea changamoto lakini changamoto hizo ziripotiwe vizuri.
Jaji alisema kuwa wao wapo tayari kushirikiana na vyombo vya habari na kwamba wataboresha utoaji habari na kuwataka waandishi kama hawajaelewa kitu kwenye kesi wawafuate ili wapewe ufafanuzi wa kilichoamriwa na si kuandika kinyume na kilichoelezwa.

Aidha alitoa wito kwa waandishi kuwa na utaratibu wa kushirikiana na mahakam pale wanapoona kuna habari inayotakiwa lakini haipatikani.
Pia alisisitiza waandishi kuandika habari za mahama kwa usahihi ili jamii iweze kurudisha imani kwa mahakama zao kwa kuwa mahama haifanyi siasa na hakuna siasa kwani wao wanadiri na sheria.

Hata hivyo katika mafunzo hayo ya siku mbili waandishi wa habari kupitia Baraza la habari Tanzania MCT walitoa maadhimio kwa Mahakama ambapo katika maadhimio hayo waliomba mahakam kwa ushirikiano na MCT kujenga utaratibu wa kuandaa mafunzo ya mara kwa mara.

Aidha waliwaomba Majaji pindi wakishasoma hukumu watoa nakala za hukumu hizo ili ziweze kuwasaidia waandishi wahabari ili kuweza kuandika habari sahihi.

No comments:

Post a Comment