Wednesday, November 25, 2015

FAMILIA YA MTOTO ALIYESINGIZIWA KUBEBA BOMU YADAI BILIONI 32

Familia ya mtoto wa Kiislamu aliyekamatwa baada ya kubuni na kutengeneza saa yake na kuipeleka shuleni kisha kudahiniwa kuwa amebeba bomu, wanadai fidia ya dola milioni 15(sawa na takribani shilingi bilioni 32 za Kitanzania)

Familia ya Ahmed Mohamed pia wanadai kuombwa radhi na jiji la Irving pamoja na shule baada ya kijana huyo wa miaka 14 kukamatwa na polisi mwezi wa tisa mwaka huu.

Kwa mujibu wa gazeti la NY Daily, mwanasheria anayewakilisha familia hiyo alituma barua katika jiji la Irving, lililoko mashariki mwa Dallas pamoja na shule ya Wilaya ya Irving Independent School nchini Marekani, akielezea kuwa mwanafunzi huyo wa darasa la tisa alisingiziwa na kukamatwa kisha kuwekwa rumande na kuhojiwa bila wazazi uwepo wa wake.

Familia ya Mohamed inalidai jiji dola za Marekani milioni 10 (sawa na takribani shilingi za Tanzania bilioni 21) pamoja na shule ya wilaya hiyo dola milioni 5(sawa na shilingi za Tanzania Bilioni 11) lasivyo watafungua kesi ndani siku 60, barua hiyo ilieleza.

BOFYA KUONA KAZI YA MTOTO HUYO. . .

Familia ya mtoto huyo wa kiume ilisema mwezi uliopita kuwa wanampango wa kuhamia nchi ya Qatar na kwamba wamekubali maombi ya tasisi ya Qatar ya mtoto wao kusoma katika chuo cha ubunifu kutokana na uwezo wake.








No comments:

Post a Comment