Bi. Samia alilazimika kusimama eneo ambalo wanawake walikuwa wamefurika wakichota maji kwa zamu huku kila familia ikipewa idadi ya ndoo kumi mara moja kwa kila wiki kiwango ambacho akinamama wengi walisema akikidhi mahitaji kwa familia zao.
SOMA ZAIDI. . .
Mgombea huyo wa CCM aliwahakikishia akinamama hao kuwa yeye kama mwanamke anajua shida ya maji inavyowatesa akinamama katika familia ikiwa huduma hiyo inapokuwa tatizo katika upatikanaji wake, hivyo atalisimamia suala hilo. Alisema Serikali ya CCM itakapoingia madarakani imetenga shilingi bilioni 13 kwa ajili ya kupeleka maji eneo la Longido mradi ambao utamaliza kero ya maji eneo hilo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Longido Bi. Suluhu alisema kwa kuwawezesha wafugaji wa eneo hilo wamepanga kujenga mabwawa ya kuvuna na kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya nyakati za ukame kwa baadhi ya maeneo, ikiwa ni pamoja na kujenga majosho ya mifugo na kuwezesha madawa ya mifugo kwa wafugaji ili kuwaendeleza.
"...Kazi hii tutaifanya ndani ya kipindi kifupi mara tu baada ya kufanikiwa kurudi madarakani, Serikali inayomaliza muda wake imefanya mengi na sisi tutaendeleza na kuboresha zaidi. Alisema wanajua kilio cha mahakama katika wilaya ya Longido hivyo mara baada ya kuingia madarakani wataijenga.

Alisema akiwa njiani katika mikutano ya kampeni zake ameshuhudia uwepo wa ukame katika vijiji lakini anawahakikishia hakuna mwananchi ambaye atakufa na njaa endapo hali hiyo ya ukame itaendelea, kwani serikali ya CCM katika ghala la chakula ina akiba ya kutosha.
Mgombea huyo mwenza wa CCM pia alifanya mkutano wa hadhara katika Jimbo Monduli aliwaomba wanaMonduli kumpigia kura ya ndio mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli ili aweze kutekeleza ilani ya chama hicho ambayo pia imejumuisha ujenzi wa barabara ya Sanya Juu hadi Longido na Longido hadi Mto wa Mbu wilayani Longido.
Aliwaomba wanaMonduli kumchagua mgombea ubungw wa Jimbo la Monduli kwa tiketi ya CCM, Bi. Namelok Sokoine kwani mgombea huyo anarekodi na historia nzuri ya utendaji kama alivyokuwa babayake marehemu, Edward Moringe Sokoine. Aliwaomba pia kuwachagua madiwani wa CCM ili waweze kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu.

No comments:
Post a Comment