Friday, August 28, 2015

KAMPENI: MWAKYEMBE "LOWASSA ALIDOKOA MBOGA YA WAZEE NA WATOTO"

Mwandishi Wetu Mbeya

WAZIRI wa Afrika Mashariki Dkt, Harrison Mwakyembe amemshukia Mgombea urais wa Chadema Edward Lowassa na kuwambia wananchi wa Jimbo la Kyela na watanzania kwa ujumla kuwa haikuwa raisi kwa maana alihusika na ufisadi wa Fedha za Richmond.

Dkt, Mwakyembe amesema kuwa katika ripoti yao ambayo walisoma Bungeni ilionesha wazi kuwa Lowassa alidokoa mboga ya wazee na watoto hivyo hana sifa kumpa dola.

Kauli hii ya Dkt, Mwakyembe ameitoa leo katika mkutano wa kampeni wa hadhara wa kumnadi mgombe wa CCM Dkt, John Magufuli ulioganyija kyela mjini.

SOMA ZAIDI. . .
 
"Ndugu zangu wanakyela ina maana mimi mtoto wenu nasema uongo, kwa bahati nzuri ninyi wenyewe mmenifundisha kusema ukweli, hivyo nataka niwambie kuwa hafai na amehusika kudokoa mboga ya wazee na watoto., "anasema Dkt, Mwakyembe

Amesema kuwa anamjua vizuri Mgombea huyo na huwezi kumlinganisha na Dkt, Magufuli kwani mgombea wa CCM anasifa, mwadilifu na ni mchapakazi.

Kwaupande wake Dkt, Magufuli amewaeleza wananchi wa Jimbo hilo kuwa amesukumwa kugombea urais kwa sababu anataka kuwatumikia na watanzania na wakimchagua na kufanikiwa kuunda Serikali basi hapo ni kazi tu.

Dkt, Magufuli leo anahitimisha ziara yake ya kampeni katika mkoa wa mbeya kwa kufanya mkutano mkubwa kuazia saa 10 jioni na kesho anaendelea na mikutano yake katika mkoa wa Njombe.


No comments:

Post a Comment