Thursday, June 05, 2014

BREAKING NEWS: JOKA LAIBUKA NA KITAMBAA CHENYE MAANDISHI YA KIARABU ARUSHA (VIDEO)


Inadaiwa nyumbani kwa mtu mmoja(jina tunalo) jijini Arusha, eneo la Sakina kaibu na Hotel 2000 (pichani) ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya clearing and forward kumetokea joka kubwa lenye kitambaa chenye maandishi ya kiarabu.

Tendo hilo limetokea muda mchache kutokea sasa kama video inavyoonesha hapo chini, mwandishi wa immamatukio aliyeongea na walioshuhudia tukio hilo wanadai kuwa, wafanyakazi waliona joka limewatokea wakati wanaendelea na kazi zao za kawaida za usafi ndani ya nyumba hiyo, wakataharuki na kutoka nje na kulifungia ndani ya geti.

Akiongea mmoja wa mashuhuda ambaye hakutaka kutajwa jina alisema kuwa "chatu alitokea chumbani kwa mama mwenye nyumba, ghafla akaenda kwenye maua, tulimpigia mwenye nyumba akasema tusimuue nyoka huyo kwani ni mtoto wake" 

BOFYA HAPA CHINI KUONA VIDEO

Hata hivyo nyoka huyo hakumdhuru mtu yoyote. angalia video kuona kilichoendelea





No comments:

Post a Comment