Monday, March 10, 2014

YANGA IMEKUFA KISHUJAA ALEXANDRIA DHIDI AL AHLY


Timu ya Yanga African imetolewa katika mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika kwa mikwaju ya penaltI katika mechi baina yake na Al ahly ya Misri ikiwa ni mechi ya marudiano iliyochezwa jijini Alexandria, ambapo katika mechi ya kwanza ilichezwa jijini Dar Es salaam.

Kufuatia ushindi wa Yanga wa bao 1 – 0 Dar es Salaam, timu hizo zililazimika kwenda kwenye penati baada ya Al ahly kushinda bao 1 – 0, na kusababisha sare. Katika penati, kipa wa Yanga Deogratius Mushi aliweza kupangua penati mbili na kuipa matumaini ya ushindi timu hiyo.


Hata hivyo Yanga ilipoteza penati 3 katika mikwaju yake. Kwa matokeo hayo Ynaga wametolewa katika mashindano hayo ya kumtafuta bingwa wa Afrika, hivyo kuipa nafasi Al ahly kusonga mbele.


Mpaka mchezo unakwisha Al ahly walishinda penati 4 – 3 thidi ya Yanga. Waliokosa penati kwa upande wa Yanga ni Oscar Joshua, Mbuyu Twite, na Said Bahanuzi.


No comments:

Post a Comment