Wednesday, March 19, 2014

WATANZANIA 3 WANASWA NA DAWA ZA KULEVYA KENYA

Watanzania wanne juzi walifikishwa katika mahakama ya Kibera ambapo walikiri kosa la kusafirisha dawa za kulevya. Wanawake watatu na mwanaume mmoja walifunguliwa mashtaka kila mmoja kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya.

Twayba Hashim alimweleza jaji wa mahakama hiyo Lucas Onyina kuwa mwezi machi tarehe 13, katika Unwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta alisafirisha dawa aina ya heroin zenye uzito wa gramu 455.4 zenye thamani ya shiling za Kenya 1,138,500. (sawa na shilingi za Kitanzania 21,521,788.45)

Tina Martin Kway(PICHANI) alikiri kubeba gramu 382.1 za madawa aina ya heroin yenye thamani ya shilingi za Kenya 955,250 (sawa na shilingi za Tanzania 18,057,697.33). Naye Omary Said alikiri kubeba gramu 664.4 za dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya shilingi za Kenya 1,661,000(sawa na shilingi za Tanzania 31,398,937.74)

Rehema Ramadhani alikubali kubeba gramu 767.5 za dawa aina ya heroin zenye thamani ya Shilingi za Kenya 1,918,750 (sawa na 36,271,349.66 za Tanzania) Hata hivyo Mwendesha Mashtaka Inspekta Imaana Mugambi aliiambia mahakama kuwa ushahidi haujakamilika.

Alisema watu hao wane walikamatwa alhamisi (13/03/2014) nab ado wanachunguzwa kama wataendelea kutoa dawa zaidi. Washtakiwa wote walidaiwa kusafirisha dawa hizo kwa kumeza na kuhifadhi tumboni.

Mugambi aliomba kesi hiyo kusogezwa mbele mpaka atakapo kamilisha uchunguzi ambapo atawakilisha kete za dawa za kulevya zilizopatikana pamoja na hati ya mashtaka.

Onyina aliamuru washtakiwa wote wanne warudishwe rumande katika kituo cha polisi cha JKIA mpaka Jumanne (jana), ambapo ushahidi utakuwa tayari kuwakilishwa mahakamani. Keshi hiyo ilitajwa jana, Imma Matukio itakufahamisha mwenendo mzima.



No comments:

Post a Comment