Tunduru
Mkazi wa Kijiji cha Sisikwasisi Wilayani Tunduru mkoani
Ruvuma aliyefahamika kwa jina la Makelele Omary (38) amefariki dunia katika
tukio lililosababishwa na ulevi wa kupindukia.
Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa, tukio hilo lilitokea
kati ya marchi 18 na 20 mwaka huu, kabla ya mwili wake uliokotwa na wasamaria
wema machi 21 mwaka huu ulikutwa ukiwa umeharibika vibaya.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa tukio hilo lililotokea
katika eneo la makutano ya Mito Muhuwesi na Nampungu ambako inadaiwa kuwa
alikwenda kwa ajili ya kutafuta kibarua ili kumuwezesha kuihudumia familia yake
marehemu alikunywa pombe nyingi haramu aina ya gongo huku akiwa hajala chakula.
Mganga aliye uchunguzi mwili wa marehemu Omari, Dkt. Joseph
Ng’ombo pamoja na kudhibitisha tukio la kifo hicho alisema kuwa chanzo cha kifo
hicho ni ulevi wa kupindukia huku akiwa hajala chakula.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Akili Mpwapwa pamoja
na kudhibitisha kuwepo kwa tukio hilo alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea
kufanya uchunguzi wa kina ili kujiridhisha chanzo cha kifo hicho.
No comments:
Post a Comment