Friday, March 07, 2014

MWANAMKE ANYIMWA URITHI KISA ANAISHI NA VVU

Arusha

Vitendo vya kuwanyanyapaa na kutowathamini waathirika wa ugonjwa wa ukimwi miongoni mwa jamii na wanandugu bado ni tatizo kubwa hapanchini,ambapo mwanamke mmoja mkazi wa Kimandolu jijini hapa,bi ZuzyMrema(40)ametengwa na ndugu zake wa kuzaliwa na kunyimwa urithi wa mali za marehemu baba yake, akidaiwa kuwa hawezi kupewa mgao wowote kwa kuwa yeye ni mwathirika wa ukimwi na marehemu mtarajiwa.

Bi. Zuzy (Pichani Kushoto) ambaye ni mtoto wa kwanza kuzaliwa miongozi mwa wake watatu wa marehemu baba yake, mzee Thomas Mrema aliyeacha mke na watoto 21 na mali mbalimbali zikiwemo nyumba kadhaa, amekiri kuishi na virusi vya ukimwi kwa muda mrefu.

Alisikitishwa na kitendo cha wadogo zake kumtenga na kugoma kumgawia sehemu ya mali za marehemu baba yake, kwani tangu afariki dunia miaka 10 iliyopita ndugu zake hao wamemtimua nyumbani wakidai hana faida yoyote katika familia yao na muda wowote anaweza kufariki dunia kutokana na maradhi ya ugonjwa unaomsibu.

''mimi ukweli ni mwathirika wa ukimwi na hata dawa ninazotumia hizi hapa (akaonyesha makopo matatu) ila hawa wadogo zangu wamekuwa wakininyanyapaa kwa muda mrefu na kuiita marehemu mtarajiwa''alisema na kuongeza.


''hivi sasa unavyoniona sina kazi maalumu ya kufanya nimekuwa nikibangaiza kwa kuuza mbogamboga na kufua nguo za watu manyumbani ambao hunilipa ujira kidogo,marehemu baba yangu ameacha mali nyingi sana ila wamejigawia wenyewe na kunitenga mimi kwa kuwa ni mwathirika''

Alifafanua kuwa marehemu baba yake kabla ya kufariki alikuwa na jumla ya wake watatu,akiwemo mama yake mzazi ambaye yupo hai,alisema upande wa mama yake walizaliwa watoto 10 na watoto watatu walifariki dunia na kubakia saba.

Alisema wake wawili wa marehemu pia walifariki dunia na kuacha jumla ya watoto 14 na kati yao watoto wanne walifariki na kubaki 10 ambao hadi sasa bado wapo hai,huku watoto wa kiume wakikataa kumgawia mali hizo na kukataa hata kuuzwa kwa mali hizo ili wagawana fedha.

Asisitiza kuwa licha ya kulifikisha suala hilo katika ngazi mbalimbali ikiwemo ofisi ya mtendaji wa kata ,kituo cha sheria na haki za binadamu na mkuu wa wilaya ya Arusha bw Raymond Mushi ambaye kwa sasa amehamishiwa jijini dare s salaam,hakupata ufumbuzi wa suala hilo.

Mwanamke huyo ameiomba serikali,taasisi mbalimbali na mashirika yanayojihusisha na haki ya mwanamke na mtoto ,kumsaidia ili aweze kupata haki yake ya msingi kwani anahofia maisha yake kutokana na vitisho anavyovipata kwa watu wasiofahamika wakimtahadhalisha kuacha kujihusisha ,kufuatilia mali za marehemu baba yake.

Kwa upande wa mama yake mzazi, bi Rose Thomas Mrema(70) alikiri mwanae huyo kunyanyapala na ndugu zake na kusisitiza kuwa watoto wake wa kiume wakiwemo wa wake wengine ndio wanashiriki kutumia ubabe kudhulumu wenzako na kujigawia mali hizo wenyewe bila kufuata taratibu.

Alisema pamoja na uzee alionao anajipanga kulifikisha suala hilo kwenye vyombo vya sheria ili haki sawa iweze kutendeka kwa watoto wote walioachwa na marehemu mume wake,ili waweze kugawana sawa.


No comments:

Post a Comment