Wanasiasa na watu maarufu duniani wamesema hawatahudhuria mashindano ya Olympic ya walemavu 'Paralympic' ya majira ya baridi nchini Urisi yaliyopangwa kufanyika katika mji wa Sochi kutokana na hatua ya Urusi katika eneo la Crimea.
Marekani imeuondoa ujumbe wa nchi hiyo kwenye mashindano hayo yanayofunguliwa leo. Nchi nyingine za Ulanya zimetangaza hatua kama hiyo.
Hata hivyo bado haijafahamika kama timu ya walemavu ya Ukraine itashiriki mashindano hayo.
Ujumbe wa timu hiyo uliinua bendera ya nchi yao wakati wa sherehe ya ukaribisho katika mji Sochi siku ya Alhamisi lakini uamuzi kwamba watashiriki mashindano hayo au la bado haujajulikana.
Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema nchi ambazo zimesusia tukio hilo hawana nia njema(bbc).
No comments:
Post a Comment