Friday, March 07, 2014

YANGA Vs AL AHLY KUCHEZA JUMAPILI UWANJA UWANJA USIO NA MASHABIKI

Wachezaji wa timu ya Yanga, Hamisi Kiiza(kushoto) na Emanuel Okwi wakisubiri kona ambao ilisababisha goli pekee la Yanga katika mechi iliyochezwa dhidi ya Al ahly ya Misri katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, jumamosi 01/03/2014.



Timu ya Yanga itacheza mechi ya marudiano na Al ahly siku ya jumapili tarehe 9/03 saa moja usiku katka uwanja wa Al max, jijini Alexandria.

Kwa mujibu wa Rais wa TFF nchini, Jamal Malinzi, serikali ya Egypt imeamua mechi hiyo ichezwe katika uwanja ambao hautokuwa na mashabiki, yaani uwanja mtupu. Jamal Malinzi aliweka kwenye Tweeter dakika chache zilizopita(soma chini).

Yanga iliibuka mshindi katika mechi iliyochezwa jumamosi iliyopita kwa kuwachapa miamba hao wa soka goli 1 bila, katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Nawatakia Yanga mafaniki katika mechi hiyo, inawezekana kabisa kumshusha mwarabu na kufuta historia mbaya.





No comments:

Post a Comment