Wednesday, March 12, 2014

MLIPUKO WA NEW YORK, 2 WAPOTEZA MAISHA, HALI ILIVYO SASA HIVI LIVE

Polisi wa jiji la New York wanasema watu wawili wamesha poteza maisha mpaka sasa kutokana na mlipuko huko East Harlem katika jumba ambalo limeporomoka. Katika tukio hilo watu wengine 17 wamejeruhiwa vibaya, na moshi mkubwa umetanda kutokana na mlipuko huo.

Ripoti kutoka katika mtandao wa CNN zimesema, wakazi wa eneo hilo walisikia mlipuko mkubwa katika jengo hilo la ghorofa 5 katika mtaa wa 116 na Park Avenue kabla halijabomoka. Huduma zote za treni ya zinazoingia na kutoka katika kituo kikubwa cha Grand Central zimesimamishwa kutokana na tukio hilo.

SOMA ZAIDI . . .
Kitengo cha zima moto cha jijini New York kimetoa tahadhari kuwa ni hali ya hatari sana na kutangaza kuwa imepeleka askari zimamoto 198 ili wakaungane na wale wa vituo vya karibu na eneo la tukio ili kupambana na moto. 

Kwa mujibu wa televisheni ya WABC TV inayoripoti live katika eneo hilo, vituo vinavyosambaza gesi vimetakiwa kuzimwa kutokana na mlipuko huo ambao umeharibu madirisha ya majengo yaliyoko karibu na eneo hilo.
Mitaa na njia za wapiti kwa miguu katika eneo hilo zimejaa vipande vya vioo vilivyovunjika vunjika kutoka kwenye madirisha ya majengo. Shuhuda mmoja katika eneo hilo ameeleza kuwa mlipukohuo ulidondosha vitu katika makabati ndani ya nyumba yake kutokana na kishindo kikubwa.


No comments:

Post a Comment