Thursday, March 13, 2014

MCHUNGAJI APIGWA KARIBU KUFA KWA KUTEMBEA NA MKE WA MUUMINI

Mchungaji Nyathi wa kanisa la Healing Ministries kutoka Bulawayo, nchini Zimbabwe amepigwa karibu kufa na mmoja wa waumini wa kanisa lake baada ya kubambwa kuwa ana mahusiano na mke wa muumini huyo.

Akiwa ndani kwa siku mbili alipigwa mara nyingi na muumini wake Isaac Dube, Mchungaji Nyathi kwa sasa yupo katika hospitali ya binafsi ambapo anapambana kuokoa maisha yake.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja ndani ya familia, Bw.Dube aligundua mahusiano hayo baada ya kupokea simu ya mkewe na kuona ujumbe wa sms ulioonesha kuwa mkewe na mchungaji walikuwa wana mawasiliano.

“Bw. Dube alipokea simu kwenye gari mwanzo akafikiri ni ya mmoja wa watu aliowapa lifti ameisahau, lakini alipata mshtuko wa maisha aliposoma ujumbe.

SOMA ZAIDI. . .
Akisoma ujumbe huo aliona jina la mkewe na ilikuwa ni ujumbe wa mapenzi” baada ya kuona hivyo, Bw.Dube akaweka mtego na kumfuatilia mwizi wake, ambapo alifanya kwa msaada wa rafiki yake wa kike aliyejidai kuwa mke wake. Mtego wake ulifanikiwa kumnasa mchungaji huyo na kuanza kumhoji mpaka akakiri.

“Kisha akamchukua mchungaji Nyathi nyumbani kwake na kumlazimisha amwambie mkewe kuhusiana na mahusiano yake ya nje. Baada ya kukiri mbele ya mkewe, Bw. Dube alimwambia atamke neno la mwisho kwa mkewe kwani siku hiyo ndio siku yake ya mwisho kumuona mkewe.

“kisha wakaondoka kwenda nyumbani kwa Bw.Dube, ambapo mchungaji alifungiwa ndani kwa siku mbili huku akipea kipigo cha uhakika.”

Mwanamke anayetuhumiwa kuwa ndio chanzo cha tukio hilo alipoona mumewe hana dalili ya huruma kwa mchungaji Nyathi, aliwaambia majirani ambao walimsaidia kumtorosha mchunganji huyo usiku.

Kisha akapelekwa hospitali kwaajili ya matibabu na haijaeleweka mpaka sasa kama ataishi.





No comments:

Post a Comment