Wakazi wawili wa kijiji cha Shatimba, Wilaya ya Shinyanga, Mkoa wa Shinyanga wamehukumiwa kwenda jela miaka 242 gerezani na mahakama ya Hakimu Mkazi wilayani humo kwa makosa mawili tofauti ya ubakaji na unyang’anyi wa kutumia silaha.
Waliohukumiwa adhabu hiyo ni James Moshi (35) na Mathias Kalonga (40) wote wakazi wa kijiji cha Shatimba wilayani Shinyanga waliokuwa wakishitakiwa kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, kubaka na kujeruhi ambapo ilielezwa kuwa katika tukio hilo walipora kiasi cha shilingi 57,000.
Akitoa hukumu hiyo juzi hakimu mkazi wa wilaya ya Shinyanga,Thomson Mtani alisema baada ya kusikiliza kwa kina ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka imebainika wazi bila ya kuacha shaka kwamba washitakiwa wote wawili walihusika na matukio yaliyotokea mnamo Oktoba 18, 2012 huko katika kijiji cha Shatimba.
SOMA ZAIDI . . .
Mtani alisema mahakama inatoa adhabu kali kwa washitakiwa hao ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo vya unyang’anyi wa kutumia na silaha na ubakaji ambapo kwa kosa la kwanza la uporaji kwa kila mshitakiwa atatumikia adhabu ya kifungo cha miaka 60 gerezani kutokana na kufanya matukio mawili tofauti kila kosa miaka 30.
Katika kosa la pili la ubakaji ambapo waliwabaka wanawake wawili kwa zamu katika matukio tofauti kila mshitakiwa pia atatumikia adhabu ya kifungo cha miaka 60 gerezani huku mshitakiwa Kalonga akiongezewa miaka miwili mingine kwa kosa la kujeruhi kwa panga na atatakiwa kulipa fidia ya shilingi 200,000 baada ya kutoka gerezani.
Akifafanua Hakimu Mtani alisema washitakiwa wote wawili watatumikia adhabu ya kifungo cha miaka 242 gerezani ambapo mshitakiwa wa kwanza Kalonga atatumikia miaka 122 na mshitakiwa wa pili, Moshi atatumikia miaka 120 pamoja na kila mmoja kuchapwa viboko 12 matakoni ambapo hata hivyo wote wawili wamepewa nafasi ya kukata rufaa iwapo hawakuridhika na hukumu hiyo.
Awali upande wa mashitaka uliieleza mahakama hiyo kuwa mnamo Oktoba 18, 2012 washitakiwa hao wakiwa na wenzao wengine ambao hawajakamatwa walivamia nyumbani kwa Lesha Jidomela wakiwa na bunduki na mapanga ambapo walimshambulia kwa kumpiga na panga na kumjeruhi vibaya sehemu za mwili wake.
Mahakama hiyo ilielezwa mbali ya kujeruhiwa kwa mwananchi huyo pia washitakiwa walipora simu tatu za kiganjani kutoka kwa Jidomela ambapo siku hiyo hiyo walivamia katika nyumba nyingine ya Sayi Jidomela ambako walipora simu moja na shilingi 57,000 zilizokuwa ndani ya mfuko wa suruali ya Sayi.
Upande wa mashitaka uliendelea kufafanua kuwa mbali ya kuwajeruhi Jidomela na Sayi pia washitakiwa hao kwa pamoja waliwabaka kwa zamu wake za walalamikaji hao wawili kitendo ambacho ni kinyume cha sheria za nchi ambapo mwendesha mashitaka wa serikali Salome Mbughuni aliiomba mahakama hiyokutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine.

No comments:
Post a Comment