Wednesday, March 19, 2014

MPIRA UMEKWISHA YANGA 1 AZAM 1, AZAM BADO IKO KILELENI

HAMISI KIIZA AKOSA PENATI, AZAM WARUDISHA GOLI WAKIWA 10 UWANJANI
FILE PHOTO
Live kutoka U/Taifa

Katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom, leo mabingwa wa Tanzania Bara watoto wa Jangwani Yanga Afrika wameshuka dimbani kukwaana na wana lambalamba Azam FC, ambapo kipindi cha kwanza ndio kimekwisha.

Mpira ulianza kwa mashambulizi makali kwa timu zote mbili ambapo katika dakika ya 14 Yanga walifanikiwa kupata bao kupitia Didier Kavumbagu ikiwa ni baada ya kutokea piga nikupige kagtika goli la Azam.

Dakika ya 19 Yanga walipoteza tena nafasi baada ya kukosa goli la wazi kupitia kwa Hamisi Kiiza, ambapo alipata pasi ya uhakika toka kwa Oscar Joshua, lakini kipa wa Azam aliokoa.

Katika dakika ya 20 timu ya Azam FC nao walipoteza nafasi ya wazi kupitia kwa mshambuliaji wake Michael Balou baada ya kupiga shuti nje ya 18 na mpira kugonga mwamba.

ENDELEA KUSOMA. . .

Mpaka kipindi cha kwanza kina malizika Yanga wanaongoza kwa bao 1 huku Azam FC wakiambulia bila. Muda wote wa kipindi cha kwanza timu hizo zilicheza mpira wa nguvu na mashambulizi makali huku wakipoteza nafasi nyingi za wazi za kufungana.

Kabla ya kuanza kipindi cha pili mpira ulilazimika kusimama kwa dakika 10 baada ya wavu katika goli la Azam FC kufumuka na kumlazimu mchezaji wa Azam, David Mwantika kurekebisha wavu hizo zilizoachia.

Mpira uliendela katika kipindi hicho na katika dakika ya 50 Kelvin Balou mshambuliaji wa Azam alikosa goli la wazi, muda mchache baada ya kuingia na kuchukua nafasi ya Hamisi Mcha, baada ya kupata pasi nzuri toka kwa Kipre Tchetche lakini mpira ukatoka nje ya uwanja.

Katika dakika ya 58, Yanga nao walikosa goli la wazi kabisa kupitia kwa Immanuel Okwi ikiwa ni baada ya kipa wa Azam, Aishi Manula kudondoka chini lakini shuti lake lilitoka nje.

Dakika ya 70 Yanga walipata penati baada ya Said Morad wa Azam kunawa mpira katika eneo la hatari lakini Yanga walikosa penati baada ya mchezaji wake Hamisi Kiiza kukosa goli.

Mpira ukiendelea mchezaji wa Azam, Erasto Nyoni alipewa kadi nyekundu baada ya kumtolea muamuzi maneno machafu.


Dakika ya 82 Azam FC wanalambalamba wanasawazisha bao kupitia kwa Kelvin Balou aliyeingia kipindi cha pili, ni baada ya kupata pasi ya uhakika toka kwa Salum Abubakar.

Mpira umekwisha huku mechi hiyo ikiwa na sare ya bao 1-1 na kwa matokeo hayo Azam FC wanalambalamba wanaendelea kujikita kileleni kwa kuwa na point 44 na Yanga wakiwa na pointi 40 wakishika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Vodacom.


No comments:

Post a Comment