Papa Francis amemsimamisha Askofu Franz-Peter Tebartz-van
Elst wa Dayosis ya Limburg, Askofu huyo maarufu anayejulikana kama “Bling
Bishop” kutokana na utata unaozunguka aina ya maisha anayoishi.
Hii imemtokea Askofu huyo mwenye umri wa miaka 53 alipotumia
dola za Kimarekani milioni 42 (sawa na shilingi bilioni 68.8), katika jumba la kifahari
huku akidaiwa kutumia dola 15,000 (sawa na shilingi milioni 24.5) kutengeneza
bafu la kuogea pekee.
Mradi huo ulipitishwa
na aliyemtangulia na ulikuwa na thamani ya dola milioni 7.5 (sawa na shilingi
bilioni 12.2), lakini mwishowe bili hiyo ilipandishwa mpaka dola milioni 42.
Katika kitita hicho kilihusisha pia dola milioni 1 (sawa na
shilingi milioni 1.6) kwa ajili ya bustani tu. Mwaka jana zaidi ya waumini 4000
waliweka saini zao kumkosoa kwa kutumia sadaka za kanisa kuendesha maisha yake
ya gharama.
ANGALIA NA SOMA ZAIDI. . .
Anadaiwa pia aliidanganya mahakama kuhusu gharama za ndege
aliyokodisha kwenda India kutembelea jamii maskini. Papa Fransis alilazimika
kumstaafisha Askofu huyo wakati uchunguzi unaendelea.
Vatican haijasema uchunguzi huo utachukua muda gani katika
Dayosisi hiyo ya Limburg huku ikikataa kueleza kwanini hawajamuondoa kabisa
Askofu Franz-Peter.
No comments:
Post a Comment