Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa uongozi wa Klabu ya Dar es Salaam Young Africans, yenye makazi jijini, wamuandikia Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum jijini Dar es Salam kuomba kibali cha kufanya maandamano.
Barua hiyo iliyoandikwa tarehe 17march 2014 ina nia ya kuandamana kupinga kucheleweshewa maombi ya ujenzi wakiwanja chao.
Barua hiyo ambayo ImmaMatukio imeipata(PICHANI KUSHOTO), imesema maandamano hayo yataanza saa4:00 asubuhi yakitokea jengo la Yanga hadi kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala kupitia barabara ya Morogoro na Lumumba
Lengo la maandamano hayo ni kushinikiza kupata kibali cha ujenzi kabla ya mwenyekiti wao Yusuph Manji hajatoka madarakani kwani ana nia nzuri ya kijenga uwanja wa kisasa
No comments:
Post a Comment