Thursday, March 13, 2014

BREAKING NEWS:BOSS WA BAYERN MUNICH JELA MIAKA MITATU NA NUSU

Bosi wa timu ya Bayern Munich, Uli Hoeness(PICHANI) amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu na miezi sita kwenda jela na mahakama ya Ujerumani kwa kosa la kukwepa kodi.

Bosi huyo wa klabu maarufu cha mpira wa miguu nchini Ujerumani na duniani alifikishwa mahakamani hivi karibuni kwa kosa la kukwepa kodi ya zaidi ya Euro milioni 15. Imeelezwa kuwa shitaka lake lilikuwa dogo la kiasi cha Euro Milioni 3.5, lakini aliamini akisema ukweli ataondolewa mashitaka kabisa.
Imeelezwa kuwa baada ya kukubali kosa na kuongeza kuwa ni jumla ya Euro milioni 16, inadaiwa alikuwa tayari ameshachelewa.
Taarifa zilizotolewa na BBC hivi punde zimesema, Uli Hoeness mahakama ya nchini Ujerumani imetoa hukumu ya kwenda jela miaka 3 na nusu, kwa kosa la kukwepa kodi


No comments:

Post a Comment