Sunday, January 12, 2014

LIVE JINSI WAUMINI WALIVYOSHAWISHIWA KULA MAJANI KANISANI



Muhubiri wa kikristo amekuwa akiwahamuru waumini wake kula majani ili kuwa ‘karibu ni Mungu’ kabla ya kuanza kuwaombea kama wanavyoonekana pichani.

Katika mahubiri ya Mchungaji(Pastor) Lesego Daniel (Pichani kushoto) wa Rabboni Center Ministries, kundi la wa waumini walianguka chini na kuanza kula majani katika huduma yake huko Garankuwa, kaskazini mwa jiji la Pretoria nchini Afrika Kusini baada ya kuambiwa ‘mtakuwa karibu zaidi na Mungu’.

kwa mujibu wa mtandao wa The Daily Mail wa nchini Uingereza, mwenendo wake huo wa ajabu umekosolewa na maelfu ya watu pamoja na kwamba waumini wake wameapa maisha yao kuendana na mtazamo wa Pastor Lesego

Mchungaji huyo anadaiwa kutamka kuwa mwanadamu anaweza kula chochote na kuishi kwa chochote atakachokula.

“Ndio tunakula majani na tunajiskia fahari kubwa kwani huo ndio uwezo na nguvu za Mungu, na kwa nguvu hiyo tunaweza kufanya lolote” alisema mmoja wa waumini wa kanisa hilo Rosemary Phetha akiongea na Time Live, televisheni ya Afrika Kusini.

Rosemary ambaye ni msichana wa miaka 21 amekuwa akipatashida kumeza huku akisumbuliwa na  koo kwa zaidi ya mwaka lakini aliponywa baada ya kuanza kula majani.

 ANGALIA MAPICHA ZAIDI...










No comments:

Post a Comment