Sunday, January 12, 2014

MAJANGA: LIVE MAKALIO YA KUONGEZA YAMUUMBUA SUPERSTAR JUKWAANI

Mwanadada mwanamuziki maarufu K’Mitchelle(Pichani Kulia), anayekuja juu kwa kasi ya ajabu nchini Marekani alikumbwa na mkasa ambao sidhani kama atausahau kwenye maisha yake.

Taarifa zilizo enea katika vyombo vya habari na kuchapishwa katika mtandao wa beforeitsnews nchini Marekani, zilimkariri msemaji wake jana akisema “K’Mitchel alienda ku-twerk (style mpya ya kucheza muziki ya kutingisha makalio), makalio yake yakagoma kutoa ushirikiano na ndipo tulihisi kuna tatizo pale”

Msemaji wake alidai kuwa walihisi tatizo ni kubwa kupindukia pale walipoona makalio ya mwanadada huyo hayatingishiki kama ilivyo kawida yake akianza kucheza mtindo huo. Iliwalazimu kupiga simu kitengo cha dharura 911 ili kupata huduma ya kwanza kwa msaada zaidi.

SOMA ZAIDI...

Katika msimu huu wa majira ya baridi kali nchini Marekani, inadaiwa makalio ya mwanadada huyo ambayo ni ya kuongeza kwa kwa upasuaji hospitali (Implant) yalizidiwa na baridi iliyopita kiwango kinachostahili.

Huku baridi ikizidi kuwa kali na joto kushuka kufikia digiree 0, ilibidi K’Mitchel alazwe hospitali mapema asubuhi jana jijini New York baada ya kugundua kuwa makalio yake hayatingishiki hata akijaribu vipi.

Bi dada K’Mitchelle anajulikana kwa makalio yake yalivyo makubwa na mwonekano nzuri, “la sivyo angekuwa demu wa kawaida tu kama waimbaji wengine” alidai mmoja wa mashabiki wake akimaanisha kuwa makalio yake yanamsaidia kumuinua na kumuongezea mashabiki na umaarufu.

Shabiki huyo aliyekuja hospitali kumtia moyo mwanadada huyo, aliongeza “hebu pata picha ya lile tako kwa karibu”

Hata hivyo madaktari walifanikiwa kuondoa kipandikizi kilichokuwa kinampa shida mwanadada huyo na kukipasha joto mpaka kilipokuwa tayari kurudishiwa katika makalio yake tena.


No comments:

Post a Comment