Jeshi la polisi mkoani Rukwa linawashikilia watu wanne kwa tuhuma ya mauaji ya mwanamke mmoja aliyeuawa na kichwa chake kuwekwa kwenye sufuria ya kupikia ugali kasha kuwekwa kwenye uwanja wa kuchezea mpira.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Jacob Mwaruanda alisema jana kuwa tukio la kuuawa kwa mwanamke huyo Ritha Malechela (35) lilitokea mwanzoni mwa wiki hii huko katika kijiji cha Kisa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
Mwaruanda alisema kuwa awali mama huyo alikuwa anaishi na hawara yake aitwaye Josephat Chinga(32) baada ya kutoroka kwa mume wake ambaye hakutajwa jina lake, ghafla nako alitoweka katika mazingira ya kutatanisha ndipo mwanzoni mwa wiki hii walikuta kichwa chake kimewekwa kwenye kiwanja kimoja cha mpira kijiji hapo.
Mwaruanda aliongeza kuwa kichwa hicho kilikutwa kikiwa ndani ya Sufuria na pembeni yake kukiwa na barua inayosadikiwa kuandikwa na mmoja wa watuhumiwa waliomuua mama huyo.
Inadaiwa mtuhumiwa huyo aliamua kuandika barua hiyo baada ya kushindwa kulipwa ujira wake alioahidiwa baada ya kumua mwanamke huyo.

SOMA ZAIDI
Kamanda Mwarumanda alisema kuwa barua hiyo ilikuwa imeandikwa majina ya waliohusika na mauaji hayo baada ya kushirikiana na hawara wa marehemu huyo kwa lengo la kupata vinganja vyake vya mikono, ambavyo inasemekana kuwa vilikuwa na alama ya "M" ambayo hawara yake aliondoka navyo kwa madai ya kwende kutengeneza dawa ili apate utajiri mali.
Inadaiwa kuwa baada ya mauaji hayo kiwiliwili cha mama huyo kilitupwa ndani ya Ziwa Rukwa na kichwa kufukiwa chini huku taarifa zikidai kuwa hawara alikahidi kuwalipa ujira wa Sh 400,000 kwa kila mmoja aliyeshiriki mauaji hayo ndipo wauaji hao walipoamua kuvujisha siri hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, waliohusika na mauaji hayo wamekamatwa na kukamatwa ni hawara ya mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina moja la Bonge, Joseph Milumba(31) Geofrey Ndenje(27) na mwanamke aitwaye Grace Sindani (40) anayedaiwa kuwa alihusika kwenye njama hiyo kwa kumshawishi marehemu huyo kuondoka kwa mume wake na kwenda kwa hawara ili aweze kuuawa.

Watu wamekuwa afadhali hata ya mnyama unaweza ukajificha akakupita ila binadamu mmmh!
ReplyDelete