Wednesday, January 01, 2014

HII NI NOMA: DEREVA WA DAR EXPRESS AKUTWA AMEPIGA VIROBA

HIvi karibuni POLISI NA SUMATRA walifanya zoezi la kupima ulevi kwa madereva Chalinze, Mkoa wa Pwani. 

Zoezi hilo lililokuwa linalenga kukipima ulevi kwa madereva wa usafirishaji hasa kwa mabasi yaendayo Mikoani, lilikuwa na lengo la kukamata madereva waliokunywa pombe na kuendesha magari hivyo kuhatarisha usalama wa abiria, wao binafsi na watumiaji wengine wa barabara.

Hatimaye zoezi hilo lilikuwa na mafanikio baada ya madereva kadhaa kukamatwa wakiwa wamekunywa pombe na baadhi walipoulizwa walisema walikunywa pombe waliyoiita viroba.
Mmoja wa madereva (PICHANI JUU) waliokamatwa ni wa basi la DAR-EXPRESS lenye namba za usajiri T640AXL linalofanya safari zake kutoka DAR-ROMBO. Dereva huyo alibainika kuwa alikuwa amelewa kutokana na vipimo kutoka kwa police wa usalama Barabarani.

Plisi ililazimika kulizuia gari hilo na kumshikilia dereva huyo ambaye hakutaka kutaja jina alipoulizwa. Police kwa kushirikiana na maofisa wa SUMATRA waliwasilina na mmiliki wa mabasi hayo ili aleta dereva mwingine na hatimaye abiria kuendelea na safari yao.

Pongezi nyingi sana kwa SUMATRA na Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri ya kuokoa maisha ya Watanzania.

 Mmoja wa madereva akipimwa kwa kupiliza hewa ndani ya chombo maalumu kinachopima kama dereva amekunywa pombe na kwa kiwango gani, CHINI: Dereva huyo akifuatilia matokeo ya ripoti hiyo. Hata hivyo dereva huyu hakuwa amekunywa pombe

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI…


Chini: mmoja wa maofisa wa SUMATRA akikagua kadi ya gari ya moja ya mabasi waliyoyafanyia ukaguzi katika enero hilo la Chalinze, Mkoa wa Pwani

 Dereva wa basi la Abood, ambaye hakutaka kutaja jina alake akijadiliana na Trafic Police juu pichani, chini ni baada ya kufanyiwa kipimo hicho


 Juu maofisa wa SUMATRA wakijaza ripoti baada ya kumkagua dereva mmoja wapo katika zoezi hilo
Chini: Shughuli nzima ya ukaguzi inaendelea


 Chini: Picha ya basi lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyekamatwa amekunywa pombe na kuendesha gari. Basi hilo la DAR-EXPRESS lenye namba za usajiri T640AXL, linalofanya safari zake kutoka DAR-ROMBO.





No comments:

Post a Comment