Aliyekuwa mshindi wa mashinano ya F1 Michael Schumacher, yuko kitandani anapambana kuokoa maisha yake baada ya kupata ajali mbaya na kusababisha majeraha makubwa kichwani wakati akiwa katika mchezo wa Skiing (mchezo wa majira ya baridi wa kuteleza kwenye barafu)
Kwa mujibu wa Daily Mail online, mshindi huyo wa mara 7 wa dunia katika mchezo wa F1(mashindano ya magari), alidondoka huko Meribel, eneo la mapumziko lililoko katika miinuko ya milima iliyoko Ufaransa
Vyanzo kutoka kwa madaktari vimeeleza kuwa Schumacher amepata matatizo kwenye ubongo. Schumacher mwenye umri wa miaka 44 aliteleza pembeni ya njia alipokuwa na mwanae wa kiume Mick mwenye umri wa miaka 14.
Michael alikuwa amevaa helmet ya kulinda kichwa alipopiga kichwa kwenye jiwe kubwa. Hata hivyo alikimbizwa kwa kutumia helikopta katika hospitali ya Grenoble, iliyoko maili 80 magaribi kutokea eneo latukio huku akiwa hana fahamu.

Lakini katika ripoti iliyotolewa jana saa 1.20 jioni, daktari alisema hali yake inaendelea kuwa mbaya, wataalamu wa ubongo na uti wa mgongo waliingia jana jioni kwaajili ya kusaidiana kuokoa maisha ya mwanamichezo huyo maarufu.
Mjerumani huyo ambaye alistaafu mchezo huo mwaka 2012, ni dereva mzuri kuwahi kutokea. Mkurugenzi wa Meribel alidai kuwa Schumacher alipatwa na mshtuko na mtikisiko.
TAZAMA PICHA ZA MICHAEL SCHUMACHER NA ENEO LA TUKIO...
Eneo aliloanguka, chini akiwa na mkewe Corina, 2008
Helikopta ikiwa mbele ya hospitali ya Grenoble alipolazwa Schumacher, Chini Schumacher akishangilia ushindi wake mwaka 2002 katika French Formula One Grand Prix
akiwa katika mwendo mkali Schumacher kwenye gari Mercedes katika Australian Formula 1 Grand Prix
No comments:
Post a Comment