Mbunifu wa mavazi nchini, Martin Kadinda(KULIA) amekanusha kupokea ujumbe kutoka kwa mwanadada Jackie Clifford 'Cliff' FitzPartrick(KUSHOTO) aliye kamatwa Desemba 19 mwaka huu kwa madai ya kusafirisha dawa za kulevya huko Macao nchini China.
Martin ambaye inadaiwa alishawahi kuwa meneja wa mwanadada huyo amekanusha uvumi wa kupokea ujumbe ambao umesambaa kwenye mitandao.
Ikiwa ni siku chache tangu kukamatwa kwa mwanadada huyo, ujumbe uliodaiwa kuandikwa na Jackie kama wosiwa kwa Kadinda, ulisambaa na kusababisha kuwa ndio majadiliano kwenye mitandao ya kijamii.
Ujumbe huo uliosomeka "Ikitokea nimekufa wosia Martin Kadinda ana maagizo yangu nini cha kufanya dont ask pls".
Akifanya mahojiano maalum na mtandao mmoja nchini, Martin aliweka wazi kuwa ujumbe uliosambaa katika mitandao ni kweli uliandikwa na Jackie lakini ilikuwa ni mwaka 2010.
Alidai kuwa ujumbe huo uliandikwa na mwanadada huyo uliokuwa ukimaanisha mambo yao binafsi na hakuna uhusiano na jambo lililotokea sasa.
Katika mahojiano hayo Martin aliweka wazi kuwa hawezi kuzungumza suala la kukamatwa kwa mwanadada huyo kwani yeye si msemaji.
No comments:
Post a Comment