Sunday, December 29, 2013
HATARI: MAJENGO HATARINI
Wakazi wa jijini wakipita pembeni mwa nyumba zilizoko pembezoni mwa barabara ya Yombo Buza karibu na kituo cha Shule, jijini Dar es Salaam Wilaya ya Temeke, kama zilivyokutwa na kamera yetu hivi karibuni, zikiwa hatarini kudondoka kutokana na mmomonyoko wa udongo uliosababishwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni. Eneo hilo lilikumbwa na hali hiyo baada ya upanuzi wa barabara. Imedaiwa wakazi wa eneo hilo wamelipwa fidia lakini wamegoma kuhama ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo. (picha kwa hisani ya Mdau wa Matukio)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment