Singida
Watu wawili wamekufa katika matukio mawili tofauti yaliyotokkea juzi Mkoani Singida likiwemo la mfanyabiashara kujipiga risasi kichwani na mwingine huchinjwa shingoni na kutolewa koromeo na ulimi.
Hayo yalielezwa na Kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishina Msaidizi Mwandamizi Geofrey Kamwela alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake mjini Singida jana alasiri.
Katika tuio la kwanza ambalo limezua msisimko na gumzo kwenye nji wa Singida Kamanda huyo alisema Mfanyabiashara Mashaka Omari (30) alikutwa chumbani kwake juzi mtaa wa Ipembe akiwa amefariki Dunia baada ya kujipiga risasi kichwani na kufa papo hapo.
Marehemu ambaye ni mkazi wa mtaa wa huo mjini hapa anasadikiwa kufanya kitendo hicho cha kutoa maisha yake kwa kutumia Bastola yake Namba TZ CA 895101 kwenye nyumba yake ya kutunzia vifaa vya ujenzi.
“Katika eneo hilo la tukio lililokaribu na nyumba ya kulala wageni ya Meatu Guest House ambapo Bastola hiyo ilikutwa pia kulikuwa na ganda moja la Risasi na vilevile magazine yenye risasi 11”. Alisema Kamanda Kamwela.
Alibaini kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa marehemu Mashaka Omari alikuwa na mgogoro kati yake na mtu mwingine ambaye hakutajwa kwa ajili ya masuala ya kiusalama kitu kilichosababisha yeye kujiua.
“Marehemu aliacha ujumbe huo wa maandishi kwenye gari lake namba T664 EES aina ya Toyota RAV IV likiwa limegeshwa nje ya ofisi yake karibu na soko kuu la Mjini Singida” Alisema Kamnda huyo.
Aliongeza kuwa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kuhusu Kifo hicho na maandishi hayo yaliyopatikana ,kisha kuwaomba ndugu wa marehemu na wananchi kwa ujumla kuwa watulivu wakati zoezi hilo linaendelea.
Katika tukio la pii lililotokea siku hiyo saa 1:30 asubuhi mkazi moja wa Kijiji cha Sambaru Wilaya ya Ikungi Tatu Selemani (42) amefariki Dunia baada ya kuchinjwa shingoni kwa kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana.
Kamanda Kamwela alieleza kuwa licha ya kuchinjwa shingo yake, marehemu alitolewa koromeo, ulimi , kuchunwa ngozi ya usoni na kutolewa sikio la kushoto, mwili wake ukiwa umbali wa meta 80 kutoka nyumbani kwake.
Alisema katika tukio hilo la Kinyama na kusikitisha mtu mmoja Amosi Shenan maarufu kwa jina la Babu mkazi wa kijiji ambaye ni mme wa marehemu amekamatwa kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kifo hicho, na uchunguzi zaidi unaendelea.
No comments:
Post a Comment