HOFU YATANDA, NINI HATMA YA MISRI
Jeshi la Misri limeng’oa madarakani rais wa kwanza kuingia madarakani kidemokrasia, Bw. Mohammed Morsi(Kushot) Bw. Morsi aliingia madarakani miezi 12 iliyopita kwa kuchaguliwa kidemokrasia nchini Misri baanda ya kupinduliwa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Bw. Hosni Mubarak(Pichani Kulia akiwa jela).
SOMA ZAIDI...
Maelfu ya waandamanaji walikusanyika katika eneo la Tahir Square
kumshinikiza Rais Morsi kuondoka madarakani lakini alikataa.
Hata hivyo Mohammed Morsi alikaidi agizo la masaa 48 lilitolewa na jeshi
la nchi hiyo la kutafuta suluisho kufuatia maandamano hayo, lakini muda huo
uliisha bila ya kupatikana ufumbuzi wa tatizo.
Jana jioni kundi kubwa la wanaompinga Bw. Morsi walisikika wakishangilia
katika jiji la Cairo, eneo la Tahir Square baada ya kutangaziwa na kiongozi wa
upinzani huku akiongozwa na jeshi kuhusiana na kujiuzulu kwa rais huyo.
Jeshi limesitisha katiba ya nchi hiyo na kuikabidhi nchi kwa Jaji Mkuu wa nchi hiyo. Jaji Mkuu huyo
ataapishwa kama rais na kutakiwa kuahidi kuitisha uchaguzi wa kidemokrasia wa
kuchagua rais mwingie.
Wakati viongozi wa serikali ya Bw. Morsi pamoja na Morsi mwenyewe wakiwa
chini ya ulinzi mkali, Rais wa Marekani Barack Obama ameonyesha wasiwasi wake
kuhusiana na kitendo hicho na hatma ya nchi hiyo na kusema ni muhimu Misri
kuongozwa na serikali ya kiraia.
Bw. Obama alikataa kusema kama ni serikali ya Bw. Morsi au ya aina gani
inatakuwa kuingia au kurudi madarakani. Naye katibu mkuu wa umoja wa mataifa
Bw. Ban Kimoon amewataka wananchi wa Misri kuwa watulivu katika kipindi hichi.
No comments:
Post a Comment