Thursday, July 04, 2013

MWANAMUZIKI WA KRISSKROSS AFARIKI AKIWA NA MIAKA34




Kris Kross' Chris Kelly na Chris Smith walipokutana mwezi februari katika miaka 20 ya studio ya So So Def Records.


Mwanamuziki wa kundi la Kriss Kross amefariki dunia kwa matumizi ya dawa za kulevya ambayo ni pamoja na heroin na kokein, kwa mujibu wa taarifa ya madaktari iliyotolewa jana jumatano.

Kris Kross, November 1992, Chicago
Chris Kelly, 34, amefariki katika hospitali ya Atlanta nchini Marekani baada ya kukutwa hajielewi nyumbani kwake mapema  mwezi mei polisi walisema.

Kwa mujibu wa mtandao wa CNN, mchunguzi wa hospitali ya Fulton County, alidhibitisha kifo cha Kelly na kwamba ilikuwa ni mchanganyiko wa sumu ya heroin, kokain, ethanol na hydrocodone, na alprasolam, kwa mujibu wa  msemaji wa hospitali hiyo Karleshia Bentley
Chris Smith, kushoto na Chris Kelly mwaka 1992.
Baada ya kuchukuliwa na gari la wagonjwa (ambulance) kupelekwa hospitali, mwanamke aliyejitambulisha kama rafiki yake Kelly, alimwambia mchunguzi kuwa Kelly alitumia mchanganyiko wa heroin na kokein, na kwamba alimpleka Kelly nyumbani ili ‘kuzinduka kwenye matumizi ya madawa ya kulevya’

Kelly, pamoja na Chris Smith waliibuka 1992 na nyimbo iliyopata umaarufu mkubwa ya Jump na kushika nafasi kwa zaidi ya wiki nane ikiongoza chati ya nyimbo 100 za Billboard


Wasanii hao pia walishirikiana na Mfalme wa musiki wa Pop, hayati Michael Jackson mwaka 1992 katika ziara ya yake ya dunia maarufu kama Dangerous.

Kriss Kross walipata umaarufu pia kutokana na mitindo yao ya mavazi ya kugeuza nguo nyuma mbele katika kipindi hicho na kusababisha vijana wengi kufuata mitindo hiyo.

Walivumbuliwa Sokoni
Viaja hao walikuwa na umri wa miaka 13 mwaka 1991 walipoibuliwa na producer Jarmaine Dupri katika super market ya Atlanta.

Wakajipa majina Mac Daddy (Kelly) na Daddy Mac(Chris), walitoka na mwimbo mwingine baada ya Jump na kuwa maarufu ukiitwa ‘Warm It Up”

Nyimbo hizo mbili zikaisukuma albam ya sokoni iliyojulikana kama “Totally Krossed Out” na kupata mafanikio makubwa. KrissKross walitoka tena na albam ya Da Bomb mwaka uliofuata 1993.

Albam hiyo haikufanya vizuri sababu watoto hao walikua na kufikia umri wa kubalehe na kulazimika kutangazwa kwa kutumia nguvu kubwa sana, kutokana na mabadiliko makubwa ya miili yao.

Taaluma yao haikuweza tena kukua na kufikia kiwango walichokuwa mwaka 1992, lakini waliendelea kutengeneza muziki. Mwaka 1996, walitoa tena albam nyingine “Young, Rich and Dangerous”

Kundi hilo liliungana tena mwezi february 2013 katika sherehe ya Jarmaine Dupri ya kampuni yake ya kurekodi muziki ya So So Def


No comments:

Post a Comment