MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Rehema Chalamila 'Ray C' a.k.a Kiuno bila mfupa amewaandikia mashabiki wake barua ya kuwashukuru kwa ushirikiano waliomuonyesha kwa kipindi chote ambacho alikuwa anafanya muziki.
Barua hiyo ambayo aliituma kupitia ukurasa wake wa Instagram ilisomeka "Nawapenda sana mashabiki wangu walionisapoti tangu miaka hiyo hadi leo, Thank u so much for ur support Hugs & kisses Ray C"
Baada ya barua hiyo kutumwa kwa kupitia ukurasa huo, iliibua hisia kwa baadhi ya mashabiki huku baadhi yao wakionekana kumuhitaji tena kwenye muziki kutokana na umahili wake wa kulimiliki jukwaa.
Ray C ni miongoni mwa wasanii wachache wa kike ambao waliotamba kwenye gemu la muziki kipindi cha miaka ya 99, huku mashabiki wake waliamua kumpa jina la kiuno bila mfupa kutokana na umahili wa kukatika kiuno pindi awapo jukwaani.
Ray C ambaye inasemekana aliathirika na matumizi ya madawa ya kulevya, hivi sasa hali yake inaonekana kuimarika.
No comments:
Post a Comment