Tuesday, June 11, 2013

WAREMBO REDD'S MISS KILIMANJARO WAINGIA KAMBINI


JUMLA ya warembo 12 wa Redd's Miss Kilimanjaro wameingia kambini kwa ajili ya kujianda na kinyang'anyiro hicho kinachotarajiwa kufanyika Juni 15, mwaka huu.Warembo hao wameweka kambi katika hoteli ya Hugo iliopo nje kidogo ya mji wa Moshi.Mrembo aliyekuwa akishikiria taji hilo mwaka jana ni Anande Michael.



Akizungumza na Waandishi wa Habari jana, Mratibu wa Mashindano hayo, Mkurugenzi wa Kampuni wa Rick Plan Company Ltd, Jackline Chuwa alisema ameamua kuwaingiza warembo kambini mapema ili kuhakikisha kuwa mashindano ya mwaka huu yanakuwa tofauti na ya mwaka jana.

“Warembo wameingia kambini mapema ili kuhakikisha kuwa mashindano yanakuwa ya kipekee, tumeboresha mambo mengi na lengo ni kumpata Redds Miss Tanzania 2013, warembo wapo Hugo Hotel,” alisema Chuwa.

Mkurugenzi huyo alisema mashindano ya mwaka huu yatafanyika Juni 15 mwaka huu, kuanzia saa moja kamili jioni katika ukumbi wa La Liga Carnivore na kuongeza kuwa viingilio ni sh. 15,000 kwa viti vya kawaida n ash. 30,000 kwa viti vya watu maalum (VIP).


Kuhusu Burudani, Mkurugenzi huyo aliwataja wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na JB, msanii wa kimataifa kutoka Burundi, Kidumu na Bendi yake, Ngoma za asili na Sarakasi huku mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.

Redds Miss Kilimanjaro 2013 inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redds Original, Panone and Company Ltd, Bonite Bottlers kupitia kinywaji baridi cha Cocacola na maji ya Kilimanjaro, Mr. Price, Hugo Hotel na Kilimanjaro Express Bus.



No comments:

Post a Comment