Saturday, June 01, 2013
MWILI WA NGWAIR KUWASILI KESHO, WATANZANIA WAISHIO AFRIKA KUSINI KUMUAGA LEO
Mwili wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea 'Ngwair unatarajia kuwasili kesho mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ukitokea Afrika Kusini
Mwili huo ambao ulitakiwa uwasili leo imeshindikana kutokana na watanzania waishio nchini humo wameomba wapate nafasi ya kuuwaga mwili huo.
Kwa mujibu wa msemaji wa kamati ya mazishi Adam Juma alisema kutokana na hali hiyo hivyo ratiba imebadilika na hivyo mwili huo utawasili siku ya Jumapili, na kuagwa siku ya Jumatatu katika viwanja vya leaders na kwenda kuzikwa siku ya Jumanne nyumbani kwao Morogoro
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment