Ikulu ya Marekani ‘White House’ kupitia ofisi ya habari imetoa taarifa ya
kuja kwa Rais wa Marekani nchini Tanzania. Taarifa hiyo ilidai kuwa Rais na
mkewe wanategemewa kutembelea nchi tatu tu za Afrika.
Katika taarifa yake iliyotumwa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na kuwekwa kwenye mtandao wa Twitter, ilieleza ziara ya Rais Obama katika nchi za Afrika, na kuzitaja nchi hizo kuwa ni Senegal, Afrika Kusini na
Tanzania. Ziara hiyo itaanza mwezi ujao (juni) tarehe 26 mpaka tarehe 3 julai.
Ziara hiyo ina lengo la kutilia mkazo umuhimu kwamba Marekani ina mahusiano
mazuri na nchi zilizoka pembezoni mwa jangwa la Sahara, ikijumuisha pia na
umuhimu wa kukuza biashara na uwekezaji na ukuaji wa demokrasia na uwekezaji
katika viongozi wa baadae wa Afrika.
Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa serikali, biashara, taasisi zisizo
za kiserekali ambapo ni pamoja na vijana, ili kuongelea mikakati maalumu ya
mahusiano kuhusiana na mambo mbalimbali ya dunia.
Safari hii ina lengo la kuongeza mahusiano na ushirikiano kati ya Marekani
na watu wa nchi za Afrika katika kukuza amani na maisha salama duniani.
No comments:
Post a Comment