Monday, May 13, 2013
LADY JAYDEE ATINGA MAHAKAMANI
Judith 'Lady Jaydee' Wambura akifuatana na mumewe leo mchana katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, (picha kwa hisani ya mtandao wa GPL)
Mwanamuziki maarufu wa bongo fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam katika kesialiyofunguliwa. Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi
wa Clouds Media Group.
Jaydee alipost mwishoni wa wiki katika mtandao wa Twitter akidai kupokea na kuitwa mahakamani hapo jumatatu saa mbili na kwamba angewajulisha wafuatiliaji wake.
Kesi dhidi ya Lady Jaydee inatarajiwa kusomwa mahakamani hapo Mei 27, mwaka huu. Blog ya matukio ilimshuhudia Jaydee akiongozana na mumewe,Gardner Habash kuelekea mahakamani hapo na kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha makarani wa mahakama na kukabidhiwa hati ya mashitaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment