Thursday, May 02, 2013
DIAMOND ABWETEKA KAMA 20 PARCENT TUZO ZA KILL
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nassibu Abdul 'Diamond Platinum' kushindwa kwake kurekodi nyimbo mpya mwaka jana kumechangia kushindwa kushika chati kwa nyimbo mpya ndiyo chanzo cha kutoingia katika vipengere vingi katika kinyanga'nyiro cha tuzo za muziki za Kilimanjaro.
Diamond ambaye alinyakuwa tuzo tatu kipindi kilichopita, hivi sasa dalili zimeonesha kutamba tena kwenye tuzo hizo kwani ameingia mara mbili katika vipengele 37.
Msanii huyo kwa kuingia mara mbili, huku wasanii wenzake kama Ommy Dimpoz kuingia mara 9 katika kinyanganyiro hicho ni wazi kuwa sasa Diamond, enzi zake zimeanza kupitwa na wakati.
Akifafanua vigezo vilivyotumika kuchagua wasanii hao kwenye kinya'nganyiro hicho, mratibu wa tuzo hizo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Angelo Luhala alisema wanachokiangalia ni msanii aliyerekodi nyimbo kwa kipindi cha mwaka 2012 na ambayo imeshika chati katika redio pamoja na televisheni na kufanya akubalike kwa kipindi cha mwaka mzima.
Kutokana na kigezo hicho ni wazi kuwa Diamond, hajatoa nyimbo mpya kwa kipindi hicho na matokeo yake ametoa nyimbo tatu mfululizo kwa Novemba mwaka jana.
Luhala alisema wanaangalia msanii alichokifanya ndani ya mwaka mzima, hivyo kama akishindwa kuchanua kwa kipindi hicho, msanii huyo atakuwa amejiweka katika wakati mgumu wa kuchanua katika tuzo hizo.
Alisema kuna baadhi ya wasanii ambao wakishapokea tuzo huwa wanajisahau kitu kinachochangia kutotokea tena kwenye tuzo zinazofuata, matokeo yake wanaonekana kama walikuwa wanabahatisha katika muziki.
Akimtolea mfano msanii aliyenyakua tuzo tano kwa mwaka 2011, 20 Percent, Luhala alisema alishindwa tena kufanya vizuri katika tuzo zilizofuata kwani hakuweza kutoa kazi zilizokubalika tena kwenye jamii.
Alisema kwa baadhi ya wasanii waliotoa nyimbo kwenye kipindi cha Novemba, nyimbo hizo zitahifadhiwa kwa ajili ya kuingia katika kinyanganyiro cha tuzo zijazo.
Pamoja na hayo, Luhala alifafanua kwamba katika upande wa muimbaji bora wa kike au wa kiume, kwenye upande wa nyimbo za muziki wa kizazi kipya, wanachanganya waimbaji wote, wakongwe na wale ambao pia wanafanya vizuri na kusikika kwani hapo zinazoangaliwa msanii aliyetoa nyimbo mpya na iliyofanya vizuri zinazoendana na vigezo ambavyo ndiyo muongozo wao.
"Hatuwezi kuwabagua wasanii kwa ukongwe wao hapa, ila tunaangalia kazi iliyofanywa na iliyofanya vizuri kwa kipindi cha mwaka mzima hivyo hata ukiwa mkongwe, unahitaji pia kuendelea kuwa mbunifu na mwenye mipango endelevu," alisema Luhala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment