Thursday, May 02, 2013
NCHIMBI ATAKA WABUNGE WAPINZANI WAOMBEWE MAPEPO YAWATOKE
KUTOKANA na kile kinachoonekana bungeni kwa kukumbwa na matukio ya mara kwa mara yanayochangiwa na baadhi ya wabunge hususani kutumia lugha ya matusi hatimaye Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi amewataka wabunge wa chama cha upinzani kupewa msaada wa kiroho kwa kuombewa ili mapepo yawatoke
Nchimbi ambaye amewataka kambi hiyo ya wapinzani kuombewa ili mapepo hayo yawatoke baada ya kuonekana kutumia siasa chafu, zilizojaa uongo, za kuchafuana za kukatana kucha hali ambayo inaonyesha mashaka yawao kukabidhiwa nchini waiongoze
Aliyasema hayo wakati alipokuwa akichangia hotuba ya Waziri wa Utalii na Maliasili Balozi Khamis Kagasheki alisema kambi ya upinzani imeamua kupotesha kwani inafahamu jambo hilo kuwa katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdurahmani Kinana hajahusika na shtuma za kuuza meno ya Tembo nchi za nje
Alisema kuwa kutokana na kujua ukweli huo wa katibu mkuu huo kuwa hajahusika na jambo hilo na wao wanaonekana bado wanashangazwa kwa jambo hilo ni sawa na kulipotosha bunge na jamii inayowaangalia
Nchimbi alisema kuwa kwa sababu anaamini maswala ya kiroho na huwa anamshirikisha Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara hiyo kwa chama cha CHADEMA alimuomba mchungaji huyo kuwaombea wabunge hao wa kambi ya upinzani ili mapepo yawatoke
"Kambi ya upinzani imeanza kupotosha bunge kwa kuwa na siasa zilizojaa uchochezi, kuchafuana kukatana kucha hivyo ni vyema sasa wakaingia katika mswala ya kiroho kwa kuomba waombewe ili mapepo yawatoke" alisema Nchimbi
Kutokana na kuonekana kukereka kwa kitendo hiko Nchimbi amesema kuwa ni heri uchawi kuliko uongo kwani uongo unaweza kuangamiza taifa taifa na uchawi ni kwa ajili ya mtu mmoja mmoja
Wakati waziri huyo akiwa anachangia jambo hilo baadhi ya wabunge wa chama cha upinzani waliomba muongo wa spika na hatimaye Spika wa Bunge hakuruhusu hali hiyo na kuwataka wakae kimya kwa kutulia kwani wakati wao wabunge wa upinzani wakati wanachangia wenzao walikaa kimya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment