Friday, May 17, 2013

DAVID BECKHAM NAYE ASTAAFU SOKA



David Beckham atastaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu baada ya miaka ishirini ya kucheza soka. Beckham aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na kuiichezea timu hiyo mara 115 na mara 394 akiwa Manchester United na kushinda mara sita ligi ya Premier na Champions League.

Beckham, 38, alisaini mkataba kuichezea miezi mitano timu ya Paris St-German(PSG) mwezi wa Januari 2013. Alisema ‘nawashukuru sana PSG kwa kuni pa fursaya kuendelea kucheza lakini nafikiri sasa ni muda wangu muafaka wa kustaafu kucheza mpira katika kiwango kikubwa hivi’

Inadaiwa timu yoyote Beckham aliyochezea msimu mzima ilishinda kombe. PSG imebakiza michezo miwili kabla ya msimu haujaisha, ambapo itacheza na Brest jumamosi na Lorient tarehe 26 Mei.

Rekodi ya David Beckham's akiwa vilabu mbalimbali
  • 1992-2003: Manchester United (Mechi 356, magoli 85)
  • 1994-1995: Preston North End (kwa mkopo) (mechi 5, magoli 2)
  • 2003-2007: Real Madrid (Mechi 157, magoli 19)
  • 2007-2012: Los Angeles Galaxy (Mechi 118, magoli 20)
  • 2009-2010: Loan spells at AC Milan (Mechi 33, magoli 2)
  • 2013: Paris St-Germain (Mechi 13, hakuna goli)
Beckham, alijitolea mshahara wake na ushindi katika ligi ya Ufaransa kwenye asasi kusaidia mahitaji mbalimbali, akiwa PSG amecheza mechi 13 toka amehamia klabu hiyo jijini Paris, Ufaransa. 

Beckham mzaliwa wa Leytonstone alichezea Manchester United, Real Madrid, Los Angeles Galaxy, AC Milan na PSG, na kubeba makombe 19 pamoja na 10 ya ligi mbalimbali.


Ni mchezaji pekee wa Kiingereza kuwahi kushiriki na kushinda soka katika nchi nne tofauti.

"Ungeniuliza wakanti mdogo kama ningeweza kushiriki na kushinda katika timu kama kapteni wa Manchester United, na kuchezea nchi kubwa na vilabu vikubwa kupita vyote duniani, ningekwambia hiyo ni ndoto’ alidai Beckham

‘Nna bahati sana kufanikisha ndoto hiyo’aliongeza Beckham

Beckham alijiunga na Man United kama mchezaji chipukizi mwaka 1991, na kui=fanikiwa kuingia kama mchezaji kamili mwaka uliofuata. Na kusaini mkataba wake wa kwanza mwaka 1993
David aliweza kufikia kuwa mchezaji wa kiwango cha juu sana duniani katika mchezo wa soka akiwa huko Old Trafford, na kuwa nyota maarufu zaidi duniani na kufunga ndoa na nyota wa muziki Victoria Adams aliyekuwa akiimbia kundi la Spice Girls mwaka 1999.

Kisha akahamia Real Madrid mwaka 2003 ambapo Beckham alichezea La Liga 2007 kabla hajahamia Marekani kuchezea LA Galaxy

Aliuza kwa mkopo AC Milan wakati wa ligi ya MLS mwaka 2009 na 2010, na kukaa Marekani kabla ya kumalizia kwa kusaini mkataba wake wa mwisho na PSG.

Wiki moja iliyopita ulimwengu wa soka ulipata pigo baada ya Meneja wa Mancheter UNited Sir Alex Ferguson ambaye pia ni mlezi wa David Beckham kustaafu kuifundisha timu ya Manchester United.


No comments:

Post a Comment