David Moyes atatajwa na
Manchester United kuwa meneja mpya kurithi nafasi itakayoachwa na Sir Alex
Ferguson. Bosi huyo wa Everton amepewa mkataba wa miaka 5 kuchukua nafasi hiyo
siku moja baada ya Sir Alex kutangaza kustaafu kuiongoza timu hiyo ambayo
ameishikilia kwa miaka 27 na kuipa ushindi mara 20.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily
Mirror, katika shughuli ya makabidhiano ya mkataba, Moyes atafuatana na
mchezaji wa zamani wa Manchester United, Phil Nevile akiwa ni sehemu ya safu
yake ya uongozi.
Gazeti la Daily Mirror
lilimkariri David Gill, Mkurugenzi Mkuu (CEO) wa klabu hiyo ambaye naye
anaondoka akisema urithi wa Sir Alex Ferguson haukuwa ‘kitu kisichowezekana’
wakati Man U ikijiandaa kumtangaza rasmi David Moyes kama Meneja wake mpya.
Ferguson ndio meneja pekee
aliefanikiwa kupita wote katika historia ya soka nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment