Saturday, May 11, 2013

ATCL YASHINDWA KURUKA KIGOMA




Taarifa zilizotufikia leo kutoka kwa mmoja wa abiria ambaye hakutaka kutajwa jina lake zinasema kuwa ndege ya shirika la ndege la ATCL imeshindwa kuondoka Kigoma Airport kwenda Dar es Salaam jana. Sababu ya kushindwa huko ni kutokana na hitilafu kwenye injini moja kusababisha kushindwa kuwaka.



Inadaiwa abiria wamelazimika kutafuta njia nyingine kufika Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja na
mabasi na kutumia ndege za shirika jingine.

Shirika la ndege la ATCL lina miliki ndege moja ambayo hata hivyo miezi michache iliyopita ilishindwa kufanya safari kutokana na kupasuka kioo cha rubani. lakini pia ilishakumbwa na mkasa wa kuanguka wakati inataka kuondoka Kigoma mwaka 2012.




No comments:

Post a Comment