Wednesday, April 24, 2013

MATUKIO JIJINI DAR ES SALAAM

KAZI POPOTE
Mwanamke ambaye aligoma kutaja jina lake alipoulizwa, akiwa anasafisha gari kama alivyokutwa na kamera yetu hivi karibuni. mwanamke huyo anafanya kazi ya mlinzi katika mtaa wa Nyamwezi Kariakoo, jijini Dar es Salaam 
UJENZI WA DARAJA
Ujenzi wa daraja lilokatika kutokana na mvua zinazoendelea jijini, likitengenezwa hivi karibuni eneo la Mbagala Kuu kuelekea Kijichi. Daraja hilo limekuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo kwani hata ujenzi wake unaendelea kwa kasi ndogo sana.

USALAMA BARABARANI
 Vijana wakiwa wadandia kontena lilibebwa kwenye gari, inadaiwa vijana hao hudandia hivyo ilikupata tenda ya kushusha mizigo. pamoja na hilo udandiaji huu ni hatari kwa usalama wa watumiaji barabara na maisha yao binafsi. tukio hilo lilikutwa na kamera yetu katika barabara ya Bibi Titi jana.

USINGIZI
Kijana ombaomba akiwa amelala kama alivyokutwa katikati ya jiji na katikati ya barabara ya Bibi Titi jijini Dar es Salaam Jana

No comments:

Post a Comment