Friday, July 27, 2012

BUILDING AFRIKA YATOA SEMINA KWA VIJANA

KAMPUNI ya Building Afrika wamendaa semina itakaoyowajengea ujuzi na uzoefu Vijana kupata ajira itakayowasaidia kukabiliana na changamoto za maisha. Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw Degratius Selestin alisema kuwa, Kampuni  hiyo imeamua kundaa semina hiyo ni moja ya  mpango mkakati wakuwaunua Vijana kiuchumi.


Alisema kuwa, mpango mkakati huo utawashirikisha Vijana kutoka sehemu mbalimbali ambapo watabadilishana ujuzi na uzoefu namna yakukabiliana na changamoto za maisha.``Kampuni yetu imeamua, kufanya hivi kutokana na Vijana wengi kukaa vijiweni pasipokuwa na ajira,hivyo basi tunaamini kupitia semina itasaidia kwa kiasi kikubwa kubadilishana ujuzi na uzoefu kutoka maeneo wanayoishi``alisema.Selestin.

Hata hivyo alisema kuwa, Maeneo yatakayozungumziwa katika semina hiyo ni Kilimo.Chakula,afya,barabra na uwekezaji wa ndani na nje.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vijana Bw Muganyizi Ernest alisema kuwa, wameamua kukutana ikiwa ni moja ya harakati zakubadilishana ujuzi na uzoefu wakuondoa tatizo sugu la umaskini linalowakabili watu wengi kwa sasa.




No comments:

Post a Comment